Lebo

Ijumaa, 19 Juni 2015

Kliniki ya wanaume waliobakwa Sweden

Stockholm South General Hospital exterior
JENGO LA SOUTH GENERAL HOSPITAL

Hospitali moja mjini Stockholm nchini Sweden inatarajiwa kufungua kliniki ya kwanza ya wanaume waliobakwa.
Kuna msem maarufu usemao ukishangaa ya Musa basi utastaajabu ya firauni. Wakati hapa Tanzania wanaharakati wakihangaika kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake kiasi cha kupelekea uwepo wa dawati la kina mama katika vituo vya polisi, ukurasa mwingine umefunguliwa mjini Stockhom.
Hospitali ya South General Hospital tayari ina eneo linalotoa huduma ya dharura kwa wanawake waliobakwa ama kunyanyaswa kijinsia.
Lakini sasa imetangaza siku ya jumatano kuwa itaanza kuwalaza wavulana na wanaume kuanzia mwezi Octoba.
Takriban visa 370 vya unyanyasaji wa kijinsia miongoni mwa wanaume na wavulana viliripotiwa nchini Sweden mwaka uliopita kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
''Kile kinachoaminika ni kwamba wanaume hawawezi kubakwa '',Daktari Lotti Helstrom aliiambia redio ya Sweden.
Amesema kuwa swala la wanaume kubakwa ni miiko lakini limeongezeka kwa kiwango kikubwa bila watu kujua.
Daktari huyo amesema kuwa ni muhimu kwa wanaume kupewa huduma za dharura sawa na wanawake.
Nini maoni yako kuhusiana na suala hili, je linafaa kuigwa na hospitali za hapa Tanzania?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni