Lebo

Alhamisi, 28 Mei 2015

Utajuaje kama akili yako si nzima?...Sehemu ya 1

Afya ya akili kwa kawaida hufikiriwa kuwa ni tabia na uzoefu unaomuongoza mtu katika kufanya maamuzi sahihi tena kwa utashi usiotiliwa shaka. Hii ni kwa mujibu wa Dr.Elsie mmoja kati ya washirika katika uandishi wa kitabu kinachojulikana kama 'Health In a Changing Society'.
Kwa upande mwingine, ugonjwa wa akili hufikiriwa kuwa ni mapungufu katika mwenendo wa kitabia na maamuzi yanayohusiana na mazingira yanayomzunguka mtu. Wataalamu wa masuala ya afya huamini kwamba kila binadamu hupata kuugua katika mfumo wake wa ubongo kila siku na hii ni katika muktadha wa ishara mbalimbali kama vile hasira, msongo wa mawazo, upweke na jazba.
Kwa mfano, mtu anayenawa mikono kila wakati anaweza kuchukuliwa kama msafi katika mazingira ya kawaida. Lakini endapo mtu huyo huyo ataonekana kunawa mikono kila mara pasipo kuthibitika kwamba kuna kazi inayomfanya mtu huyo kuchafuka kila mara, basi mtu huyo atachukuliwa kuwa ana ugonjwa unaomsumbua akilini mwake.
Pia, mazingira ambayo mtu anapenda kukaa sana ijapokuwa mazingira hayo siyo ya kawaida basi aweza kuchukuliwa kuwa ana matatizo ya kiakili. Mfano, mtu anayekaa na kula katikati ya eneo la takataka. Ni wazi kwamba ugumu wa maisha na uchumi dhaifu miongoni mwa watu wa tabaka la chini huchochea magonjwa ya akili. Ieleweke kwamba ili mtu awe na ugonjwa wa akili si lazima awe mwehu au kichaa ukiachana na mtindio wa ubongo bali pia mazingira yake.
Siku hizi waweza kutana na mtu mzima akiwa na mfuko mchafu mgongoni katikati ya dampo, kwa upande mmoja aweza kuitwa 'MJASIRIAMALI' lakini afya ya akili yake ipo matatani.Anaugua mojawapo ya magonjwa yaliyotajwa katika tufe hilo hapo chini.
 
Pia watu wanaoongea wenyewe binafsi na kuonekana kama wanawasiliana na nafsi zao wanakuwa na matatizo ya kiakili yanayokuwa yanawasumbua kwa wakati huo.
Pamoja na mambo mengine, tafsiri yoyote ile kuhusu afya ya akili haikosi utata na yaweza tatizwa na muktadha wa kitaaluma kama vile saikolojia, falsafa, utabibu, imani  na mazingira.
Lakini kwa vyovyote vile, kuna fasiri zilizo bora na muhimu  zaidi kuliko nyingine.Jambo linalofuata hapa ni kupima uzani wa hoja na ushahidi wa sheria ya asili (natural law) katika kuamia lipi si ishara ya afya ya akili na lipi ni ishara.
Kwa mfano, mtu mwehu aweza kula na kunywa mabaki ya vyakula na vinywaji jalalani kwa muda wa mwezi mzima na asidhurike, lakini yule mwenye afya ya akili aweza ugua gafla ndani ya dakika chache tu. Je, wajua sababu ya jambo hili na siri ya afya ya akili?


 Afya bora ya ubongo humwongoza mtu katika kufanya mambo makuu matano yanayohusiana na ufahamu ya kama vile kuratibu kwa utimilifu wake kazi za pua, ulimi, ngozi, macho, masikio na hunchi.
Hunchi si kiungo kinachoonekana lakini hufanya kazi ya uratibu, ubunifu na ugunduzi katika ubongo wa binadamu. Kwa huu ulimwengu wa kiteknolojia twaweza sema ni software ya ubongo. Kumbe viungi vyote hivi hufanya kazi kwa kushirikiana na hatimaye kujenga mazingira ya utambuzi wa kitabia na hatua za mwonekano. Mfano, mtu kichaa aweza vua nguo zote hadharani na akatembea bila wasiwasi lakini wewe ndugu yangu hata kama umefumaniwa na mke wa mwanajeshi kisha wananchi wakakuvua nguo zote ili utembee uchi basi utakuwa ni mtihani mgumu na hata kama utaufanya na kufaulu basi baadaye ni lazima uhame mtaa.
Lakini, wewe si una mach sawa na ya yule kichaa? Kwanini macho ya ubongo wako yanakwambia jambo hilo si sahihi?
Basi ni mambo yepi siyo ishara ya akili timamu na yepi ni ishara ya akili timamu? Ni upi msaada wako kwa mtu mwenye maradhi ya akili?
Itaendelea... majibu ya maswali haya yatajibiwa katika makala itakayofuata kuhusu jambo hili.
Kwa maswali, maoni na ushauri usiache kuwasiliana nami.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni