Pamoja na mambo mengine, muktadha wa kimantiki katika dhana ya kitabibu afya huangaliwa kwa fasiri ya falsafa ya afya (health philosophy). Mtu aweza kuhoji kwanini mtu anayeishi mjini na kutumia maji ya kopo au yaliyochemshwa ataugua mara moja endapo ataenda kijijini na kutumia maji ya chemi chemi ambayo binadamu na wanyama hifadhi yao ni moja?
Lakini vile vile mtu wa kijijini akihamia mjini na kunywa maji safi ya kopo aweza kuugua japokuwa maji aliyokunywa ni safi na salama zaidi kuliko yale ya kijijini?
Kuna kitu kinaitwa 'psychic power' yaani nguvu ya maono ya ajabu ya mtu husika na kwa mantiki hiyo, afya ya mwili wa binadamu pamoja na mambo mengine ni matokeo ya maono binafsi na mantiki za kifalsafa.
Jambo lile ambalo mtu hulichukulia kwamba ni jeupe basi ni jeupe kweli kwa mujibu wa maono yao na mtu akiamini kwamba hawezi kudhurika na jambo fulani huwa inakuwa hivyo.
Kwa mujibu wa mwanasayansi na mwandishi mashuhuri, Rene Dubos katika kitabu chake cha 'Man, Medicine and Environment (1968)' anafafanua afya ya "mwili kama njia ya maisha inayomwezesha binadamu asiye mkamilifu kuishi pasipokuwa na maumivu makali wakati anapojaribu kuendana na mazingira yasiyo na usalama"
Unayaonaje mazingira ya mtu huyo hapo kwenye picha iliyopo hapo chini, je yanachochea upatikanaji wa afya mwili katika mazingira yasiyo na utimilifu?
Kati ya jambo ambalo kila mmoja linamhusu basi ni afya yake. Pamoja na sababu nyingine nyingi, ukweli ni kwamba mazingira huamua hatma ya afya ya mwili wa mtu. Ukichukua picha ya mtu huyo ndani ya shimo na huyo hapo chini kitandani tofauti ni moja yaani mandhari tu lakini hali ni moja.
Tukiachana na picha hizo hapo juu, turudi katika mazingira ya kawaida. Mtu mwenye afya njema ya mwili aweza kuwa yupi?
Nakumbuka kipindi cha umaarufu wa babu wa Loliondo ambapo maelfu y awatu walifurika kwenda kupanga foleni ili wapate dawa iliyosemekana kuwa dawa ya maajabu kwa vile ilitajwa kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa sugu kama vile UKIMWI, Kisukari, saratani na shinikizo la damu. Je, wewe ndugu yangu msomaji u mzima kwa kadri gani?
Ni lini mara yako ya mwisho kumwona daktari?
Je, unasubiri kuugua ndipo ukapime afya au huwa unapima kila baada ya muda fulani?
Ahsante kwa kufuatilia makala hii, ujumbe muhimu ni kwamba unatakiwa kupima afya yako kab la hujaugua vinginevyo unajitengenezea kahandaki ambako viini vya magonjwa vikikugundua basi utafukiwa bila taarifa.
Kwa maoni, ushauri au swali basi usikose kuwasiliana na mimi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni