
Kuna msemo maarufu mtaani usemao Mungu si Athumani, unalilia unene wa makalio kwasabababu hujawaona wanene. Unalilia wembamba kwa sababu hujawaona wembamba duniani, kumbe fahari ya macho ni uzuri wa kile alichokupatia mwenyezi Mungu na unatakiwa kushukuru kwa hilo.
Mwanamama Mikel Ruffinelli, mkaaji wa jijini Los Angeles kunako ardhi ya Marekani ndiye Mwanamke mwenye makalio makubwa kuliko wanawake wengine wote hapa duniani.
Mama
huyu wa watoto wanne amekuwa akipata shida kupitisha umbile lake la
inchi 100 kwenye mlango na anahitaji nafasi ya watu wawili kwenye ndege.
Mikel
mwenye umri wa miaka 39 anaendesha magari makubwa kwa vile mwili wake
mwenye kilo 190 hauwezi kukaa kwenye magari madogo na anahitaji kiti
chenye uimara wa ziada nyumbani.

The
Sun la Uingereza linaandika kuwa bibie huyo aliyekuwa na kilo 63
utotoni anajiskia fahari kwa umbile lake hilo na hana mpango wa
kupunguza uzito, japo kuwa wakati mwingine anapata kero. Anasema:
“Popote napokwenda, kwa uzuri au ubaya, ‘hips’ zangu zimekuwa zikwashtua
watu.
“Napokuwa mitaani nikitembea huwa naskia milio ya kupigwa picha kwa simu na kamera huku watu wengine wakinicheka.
“Baadhi
ya watu wanadhani nimefanya upasuaji kuongeza figa langu, lakini hii ni
halisi. Nadhani ni matokeo ya kuzaa watoto wanne, lakini hips kubwa
zipo kwenye familia yetu”
“Naposafiri kwa ndege au treni nalazimika kununua siti za watu wawili kwasababu makalio yangu hayataenea kwenye siti moja”.
MWANAMA
Mikel Ruffinelli mkazi wa Los Angeles, Marekani, amedhihirisha kuwa
ndiye mwanamke mwenye ‘hips’ kubwa zaidi duniani akiwa na mzunguko wa
zaidi ya futi 8.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni