
Medan, Indonesia.
Ndege ya abiria nchini Indonesia imeanguka katika jiji la tatu kwa ukubwa nchini Indonesia almaarufu Medan na kuua idadi kubwa ya watu. Kwa mujibu wa taarifa za kimtandao kutoka katika kituo cha Associated Press, zimeonekana nyufa katika ndege hiyo iliyotambuliwa kwa namba C-130 Hercules huku pia likionekana gari lililovunjwa vunjwa likiwaka moto sambamba na makazi yaliyobomolewa. Moshi mkubwa umeonekana kutoka katika eneo la tukio huku idadi kubwa ya watu ikidhaniwa kuwa wamefukiwa hapo.
Mkuu wa polisi Eko Hadi Sutedjo kutoka katika ukanda wa Sumatra ya kaskazini amewambia wandishi wa habari kuwa ndege hiyo ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 50 kwa kawaida lakini mkuu wa kitengo cha usafiri wa anga Kamanda Marshall Agus Supriatna amesema kwamba bado hakujawa na uhakika kuhusu idadi kamili ya watu waliokuwemo katika ndege hiyo kwa kuwa ndege ilisafiri kutoka katika mji mkuu wa Jakarta na kutua katika vituo vikuu viwili kunako njiani. Inaaminika kuwa, ndani ya ndege hiyo kulikuwamo na wanajeshi, ndugu zao na hata abiria wa kawaida.

Miili 37 ya watu waliokufa imekutwa na kupelekwa katika hospitali ya Medan's Adam Malik akiwemo mtoto mdogo anakadiriwa kuwa wa umri wa mwaka mmoja. Nchi ya Indonesia ina rekodi mbaya za kiusalama na kati ya mwaka 2007 na 2009 umoja wa ulaya ulizipiga marufuku ndege za Indonesia kutuambaa katika anga lake kwasababu za kiusalama.
Shuhuda mmoja amekiambia kituo cha runinga cha MetroTV kwamba rubani wa ndege hiyo awali alitoa taarifa za kurudi katika uwanja wa ndege wa Medan kabla ya ajali akieleza kuwa alihisi tatizo katika mfumo wa injini. Mji wa Medan ni wa tatu kwa ukubwa ukitanguliwa na majiji ya Jakarta na Surabaya. Indonesia ni nchi yenye wakazi wapatao milioni 3.4
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni