![]() |
Emma Morano, Tar.28 June 2015 |
Wameshuhudia kipindi ambacho msanii Mark Twain aliita zama ngumu, 'Gilded Age' na kushuhudia hatma ya harakati za haki za kiraia nchini Marekani. Pia wameshuhudia mifumo ya uongozi wa kidikteta kama ule wa Benito Mussolini, Adolf Hitler na wengine wengi. Haikinzani kuamini kuwa wanawake hao wameshuhudia chanjo ya ugonjwa hatari wa polio sambamba na kutimia kwa zilizokuwa ndoto za Mwanaharakati wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi yaani Martin Luther King Junior aliyeota ndoto kwamba, IKO SIKU MAREKANI ITATAWALIWA NA RAIS MWEUSI. Ajuza wawili wameshuhudia Rais Barrack Obama akiongoza Marekani.
![]() |
Susannah Jones, Juni 22, 2015 |
Susannah Jones anayeishi katika jiji la New York, Marekani kwa sasa ndiye binadamu aliyepata kuishi kwa zaidi ya miaka 110 kwa mujibu wa kumbukumbu zinazohifadhiwa na kituo cha utafiti wa watu walioishi miaka mingi cha jijini Los Angeles yaani 'Los Angeles-Based Gerontology Research Group. Kwa upande wa bibie Emma Morano aliyezaliwa katika mji wa Morano nchini Italia amezidiwa umri wa miezi michache na Jones. Kwa mantiki hiyo, kituo hicho hakijui taarifa nyingine zozote kuhusu uwepo wa binadamu wenye umri mkubwa zaidi ya watu hao wawili.
Ajuza Emma Morano
ameishi peke yake tangu alipoachana na mumewe mwaka 1938 kwasababu alikuwa akimpiga sana na kumnyanyasa. Anaishi katika chumba chake ndani ya makazi ya Verbania katika mwambao wa mlima Lake Major kaskazini magharibi mwa nchi ya Italia na anatunzwa na kijiji chake. Meya wa mji huo alimpatia runinga na daktari wake aliyemhudumia kwa miaka zaidi ya 25 hufanya uangalizi kila mara tena kwa uangalifu mkubwa.
Morano yeye binafsi anauchagiza ukubwa wa umri wake kuwa unatokana na mlo usiokuwa wa kawaida: anakula mlo wa mayai matatu kwa siku sambamba na gramu 150 za nyama ambayo haijasindikwa na huo ndiyo mlo wake tangu akiwa mdogo. Anaeleza Morano, "Baba yangu alinipeleka kwa daktari ili nikatibiwe maradhi ya Anemia, na daktari aliponiona alisema 'msichana mrembo hivi, ungekuja naye baada ya siku mbili tu mbele basi nisingeweza kukusaidia'." Anaeleza bibie Emma Morano kuwa daktari alimwambia ale mayai mawili au matatu kwa siku hivyo ninakula mayai mawili kila siku.
Daktari wake anasemaje?
![]() |
Emma Morano, akitazama picha ya umakamo wake siku za hivi karibuni |
Daktari Carlo Bava anasema kuwa pia kuna viini vya urithi vilivyopelekea umri huo kwa kuwa Morano haugui kila mara hivyo hiyo ni ishara ya kuwa na kinga inayojitosheleza tena kwa kipindi kirefu. Italia ni nchi maarufu sana kwa kuwa na idadi nzuri ya watu wenye umri mkuu na sasa Chuo kikuu cha Milan kinafanya utafiti kuhusu sababu za Morano kuishi umri mkubwa zaidi.
Emma Morano anapingana na kila kitu kinachoelezwa kuwa mlo kamili na lishe maalumu, yeye anakula anachokitaka tena mara nyingi kwa kujirudia tena kwa miaka mingi mfululizo. Hapendi kukaa mpweke hivyo muda ambao amakuwa peke yake anasema kuwa huwa anaimba na kukumbushia enzi zake ambapo wanaume hawakusita kusimama pale walipoisikia sauti yake. Wimbo anaoupenda zaidi ni ule wimbo maarufu wa mapenzi uitwao 'Parlami d'amore Mariu' uliopata kuvuna sana katikati mwa miaka ya 1930. "Lakini siku hizi siwezi kuimba vema", analalamika bibie Emma Morano.
Daktari Carlo Bava anaeleza kuwa umri mkubwa wa Emma pia umechagizwa na uimara wake katika maamuzi na namna anavyoyachukulia maisha. Miezi michache iliyopita alitakiwa kuongezewa damu lakini alikataa kwenda hospitali akidai kwamba hata akifa hiyo itamaanisha kwamba siku zake zimefika. Shangazi zake wanaomjali wanasema kila siku huacha biskuti na chokoleti kila siku lakini kesho yake hawakuti siku hivyo ni ishara kwamba ajuza huyo anaamka usiku kula. Kwasasa hawezi kutembea ila anamudu kujikokota kwenye kiti cha mataili na kutembea hatua fupi kwenda kitandani.
![]() |
Bi.Susannah M.Jones akila chakula |
Susannah Mushatt Jones, yeye alizaliwa tarehe 6, Julai ya mwaka 1899 na sasa na umri wa miaka 115. Alizaliwa mashambani karibu na mjini Montgomery katika jimbo la Alabama na alikuwa ni mmoja katika familia ya watu 11. Alisoma shule maalumu ya wasichana weusi na pindi alipohitimu mwaka 1922, Jones alifanya kazi sambamba na ndugu zake katika uzalishaji wa mazao shambani. Baadaye alihamia mjini New York.
Hakuwahi kuwa na watoto wake mwenyewe bali alilea watoto wa wengine licha ya kuolewa mara kadhaa. Ndugu zake wanasema hakuna sababu za kitabibu zilizopelekea umri mkubwa bali ni ile hali tu ya kupenda ndugu na kuishi kwa kujali wengine na pengine kwasababu alikulia kijijini na kula sana matunda na mboga za majani ambazo hazijachanyika na sumu ya aina yoyote ile. Kwa sasa hasikii vizuri lakini walau anapata hisia za Rais mweusi Barrack Obama.
Wiki hili atatimiza miaka 116 na familia yake inajipanga kuandaa sherehe ya siku ya kuzaliwa. Taarifa hizi zimepatikana kwa msaada wa Balsamo aliyeripoti kutoka New York na Calanni kutoka Verbania kabla ya kuandikwa katika mtandao wa yahoo na kutafsiriwa na http://lumulinews.blogspot.com.TUUNGANE KATIKA KUPIGA VITA MAUAJI YA VIKONGWE TANZANIA!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni