Lebo

Alhamisi, 11 Juni 2015

CEO kuendeleza mdahalo na wagombea urais kupitia UKAWA


Kufuatia hali ya watangaza nia kupitia CCM kukimbia mdahalo ulioandaliwa na CEO Round Table, Mwenyekiti wa CEOrt Mhe.Ali Mufuruki ametangaza azma ya taasisi hiyo kuendeleza mchakato wa midahalo kupitia watia nia wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Akieleza kusikitishwa kwake na hatua ya watia nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kususia mdahalo huo muhimu ambao ungekuwa wa kwanza tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Bwana Mafuruki ameeleza kwamba CEOrt hawajavunjika moyo.
Akijieleza kwa hisia kali Mufuruki akiongea na vyombo vya habari amesema,
“On behalf of the leadership and members of the CEOrt, we offer our heartfelt apologies to the many people who came to the debate venue, to the millions of viewers on TV, radio and internet, to our media partners and to our sponsors the Uongozi Institute,” the CEOrt Chairman Ali Mufuruki apologised in press statement released yesterday,
“We are saddened and disappointed by what happened but we are by no means discouraged. We will proceed to make arrangements for the next debate,”
Mwenyekiti Ali Mufuruki amewaomba radhi wananchi wote waliofika  ukumbini kwa ajili ya kushuhudia mdahalo sambamba na wale waliokuwa wamejiweka tayari kuangalia kupitia runinga. Zaidi ameeleza kuwa mdahalo utakaofuata utakuwa tarehe 18, junei 2015 na mdahalo wa mwisho utakuwa tarehe 25, juni 2015.

Mwenyekiti wa CEOrt, Ali Mufuruki
















                                                                       
Akizungumza na gazeti la The Guardian, Mufuruki ameeleza kuwa awali mwezi uliopita, ushirika wa umoja wa waajiri Tanzania kupitia Chief Executive Officers Round Tables (CEORT) walitangaza dhamira yao ya kusimamia zoezi la kuendesha mdahalo maalumu kwa ajili ya kuwahoji watangaza nia wa Urais kupitia CCM ili kuwapa wananchi wigo wa kuwapima sera, uwezo na maono yao kuhusu Tanzania na watu wake.

Akitamatisha taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mwenyakiti Mufuruki amekiri kuwa ni vigumu kwa taifa kubadili utamaduni wa kisiasa ambapo wagombea hawataki kukubaliana na utamaduni upya wa midahalo lakini hii ni safari na tayari imekwisha kuanza.

Kutokana na hatua hiyo iliyotangazwa na Mwenyekiti wa CEOrt, tayari wananchi wameanza kupata mwamko mpya wa kutaka kujua zaidi kuhusu ratiba ya nani na nani watashiriki katika mdahalo huo wa UKAWA huku hamasa kubwa ukiwa ni iwapo Dr.Slaa na Mhe. Lipumba watashiriki moja kwa moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni