Lebo

Jumapili, 21 Juni 2015

EXCLUSIVE...TFF imemfukuza kocha wa Taifa Stars na kumlipa fidia ya milioni 200/=tsh

 index
Ikiwa ni siku moja tu baada ya timu ya taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) kufugwa goli tatu bila majibu na timu ya taifa ya Uganda 'Uganda the cranes', Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limemfuta kazi aliyekuwa ocha wa wa timu hiyo kocha Maart Nooij pamoja na benchi lote la ufundi.
Katika taarifa ilyotolewa kwa vyombo vya habari TFF imeanisha mambo makubwa matatu kama hatua stahiki dhidi ya hali ya mbaya ya kisoka kwa timu ya taifa ya Tanzania. Pamoja na mambo mengine kamati tendaji ya TFF imetangaza:
1/Ajira ya Kocha Mkuu wa Taifa MaarjNooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015
2/Benchi lote la ufundi la timu ya taifa limevunjwa rasmi kuanzia Juni 21, 2015
3/Uongozi wa TFF utatangaza benchi jipya la ufundi.

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI

Pamoja na maamuzi hayo ya TFF wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini haswa katika mitandao ya kijamii wameelezea kukatishwa tamaa na mwenendo wa timu ya taifa huku wakiitupia lawama serikali na shirikisho la soka nchini kwa kushindwa kuweka miundombinu bora kwa maendeleo ya soka.
Pia kwa kitendo cha TFF kuvunja mkataba na kocha ina maana kwamba itamlipa fidia ya shilingi milioni 200/= fedha za kitanzania huku akiwa hajaisaidia timu hiyo kufika pahala ambapo Watanzania wengi wangefurahi.
KOCHA MAART NOOIJ SIKU ALIPOKUWA NA WACHEZAJI MAZOEZINI

Taifa Stars imekuwa na mwenendo mbaya kwa karibia mwaka mzima. Kwa mujibu ya taarifa ya kila mwezi ya viwango vya ubora wa soka vilivyotolewa na FIFA, Taifa Stars imeporomoka kutoka nafasi ya 107 mpaka 127. Kwa tathmini ya mechi za hivi karibuni, katika mechi 6, timu yetu ya taifa haijashinda hata mechi moja na katika mechi mbili za mwisho siyo tu kwamba haijashinda hata mechi mja bali pia haijafunga hata goli moja isipokuwa imefungwa magoli 6 ikiwa ni wastani wa kufungwa goli 3 katika kila mechi.
Matumaini ya watanzania kuhusu kufuzu hatua za mtoani za AFCON zimeishia ukingoni huku wengi wakijiweka kando kwa kusubiri mabadiliko ya mfumo ambao pengine utakuwa na manufaa kwa taifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni