
Hekaheka za maandalizi ya vikao hivyo kuanzia vya maadili, Sekretarieti, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa, zimeanza kuonekana wazi huku nyumba zote za kulala wageni na hoteli zikiwa zimekwishajaa kwa muda wote wa vikao hivyo.
Kumekucha na Hapatoshi mjini Dodoma.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea hali ilivyo mjini hapa, wiki mbili
kabla ya vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza kazi ya
kumtafuta mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Hekaheka za maandalizi ya vikao hivyo kuanzia vya
maadili, Sekretarieti, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano
Mkuu wa Taifa, zimeanza kuonekana wazi huku nyumba zote za kulala wageni
na hoteli zikiwa zimekwishajaa kwa muda wote wa vikao hivyo.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwenye maeneo ya
katikati ya mji wa Dodoma, umebaini kuwa nyumba za kulala wageni na
hoteli zimejaa kuanzia Julai 8 hadi 12, mwaka huu.
Hali hiyo imewafanya watu wanaotaka kupanga katika nyumba hizo kuulizwa wataondoka lini, ili tarehe za ‘booking’ zisigongane.
“Utaondoka lini, maana CCM wamechukua nyumba zote
hapa kati ya Julai 8 hadi 12,” alisema mmoja wa wahudumu katika nyumba
ya kulala wageni ya Kiramiya.
Chanzo cha habari kutoka katika ofisi ya CCM,
kimesema wajumbe wote 2,448 wa mkutano mkuu wamepata maeneo ya kulala
kwa siku watakazokuwa mjini hapa.
Hata hivyo, chanzo hicho kimedokeza kuwa
changamoto imekuwa katika kupata malazi ya wageni 600 waalikwa,
watakaokuja kuhudhuria mkutano mkuu huo utakaofanyika katika ukumbi mpya
wa chama hicho.
“Katika maeneo mengi tuliyokwenda tulikuta hoteli
zimechukuliwa na wapambe wa wagombea wa urais ambao tayari wamelipia
siku watakazokaa mjini hapa,” alisema mmoja wa wanakamati ya maandalizi
ya CCM na kuongeza:
“Hivi sasa wenzangu wako mtaani wanatafuta nyumba nyingine.”
Alisema hali imekuwa ngumu kutokana na wapambe wa
wagombea ambao hadi sasa wamefikia 39 kuchukua vyumba vingi na kuvilipia
kabisa, tofauti na CCM iliyopanga kuanza kulipia malazi hayo leo.
UKARABATI
UKARABATI
“Hujaingia humo ndani lakini ukumbi unafanyiwa marekebisho
makubwa ili mjumbe atakayekaa mwisho aweze kuona mbele kwa urahisi, siyo
kama ilivyokuwa zamani,” alisema mmoja wa makada wa chama hicho.
Nje ya ofisi hizo, wafanyabiashara wanaouza sare
za chama hicho na bidhaa nyingine za kumbukumbu za chama, wamekwishaanza
kupanga biashara zao kandokando ya ukuta wa jengo hilo wakisubiri
kunufaika na wingi wa wageni mjini hapa.
Jumla ya wagombea 39 wamejitokeza hadi sasa kuomba
nafasi ya kuipeperusha bendera ya CCM katika kiti cha urais, kwenye
uchaguzi mkuu Oktoba 25 na wengi wao wanaendelea na kazi ya kukusanya
wadhamini katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa hivi karibuni na
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Kamati ya Usalama na Maadili
itafanya kikao chake Julai 8, mwaka huu kuangalia utaratibu wa kanuni
kama haukuvunjwa.
Alisema kikao hicho kitafuatiwa na Kamati Kuu
itakayofanyika Julai 9 ambayo inatarajiwa kuchuja wagombea hadi watano,
kisha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) itakayofanyika Julai 10 ambayo
itapunguza zaidi na kubakiza wagombea watatu watakaopigiwa kura na
mkutano mkuu.
Mkutano Mkuu wa chama utafanyika Julai 11 na 12 na kumchagua mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
Kwa upande wa mgombea urais wa Zanzibar, Nape
alisema Kamati ya Usalama na Maadili ya Zanzibar, itafanya kikao chake
Julai 4, ikifuatiwa na Kamati Maalumu Julai 5.
@Mwananchi
@Mwananchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni