Unajua kila mtu ana kwao duniani, hata hawa wanaoitwa watoto wa mitaani wana kwao isipokuwa wamekosa fursa ya kukaa nyumbani kwao. Kwa hiyo hata mimi nina kwetu na kimsingi kwetu ni kule alikozikwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi aliyeuwawa na askari polisi, kijiji cha nyororo, Iringa alipokuwa katika majukumu yake ya kitaaluma mnamo mwaka 2012.
Sasa kule kwetu Mbeya, halmashauri ya Busokelo mwaka 1998 kuliwahi kutokea msiba. Mtoto wa Mzee Mwakhibigo alikufa maji mtoni alipokuwa akijaribu kumwokoa kijana mwenzake aliyejulikana kwa jina la Ndabhiti Mwalubigo katika mto Lufilyo. Ilikuwa ni mwezi wa nne ambapo kunakuwa na mvua nyingi maeneo mengi ya mkoa wa Mbeya.
Sasa tukio lilikuwa hivi: Atupele Mwakhibhigo na Ndabhiti Mwalubigo walitoka msituni katika safu za mlima livingstone wakipita kijiji cha Matamba wakiwa na 'Mapapati'. Mapapati ni magamba yatokanayo na mianzi ya mwituni yanayotumika kuezekea nyumba za asili. Kipindi cha masika ndipo mapapati hupukutika kwa wingi hivyo vijana wengi hufanya shughuli hiyo kwa ajili ya kuezekea nyumba zao au kuuza na kujipatia kipato cha kujikimu.
Sasa walipofika katika 'lulalo' au daraja tena la mti mmoja Ndabhiti Mwalubigo aliona wingu kubwa likija kutoka upande wa juu, kutahamaki alipata kizunguzungu gafla kisha alitumbukia mtoni.
Atupele alipogeuka gafla alimwona mwenzake akinywa 'vikombe' vya kutosha mtoni. Akatupa huko mzigo wake kisha akaogelea kwenda kumwokoa rafikiye, alijitahidi kupambana na hatimaye alimwokoa. Walipokuwa wamepumzika na Ndabhiti kupewa huduma ya kwanza basi waliafikiana waendelee na safari. Kwa kuwa Atupele Mwakhibigo alijua fika kwamba mwenzake alikuwa amechoka basi alimtwisha mwenzake mzigo. Aligeuka ili naye ajitwishe na ndipo alipogundua kwamba 'ikhitili' yaani kofia yake ya mkeka ilikuwa inaning'inia kwenye miiba kumbe ilichopoka alipokuwa katika harakati za kumwokoa rafikiye.
Basi Ndabhiti alimwamuru rafikiye atangulie mbele hali yeye akifata kofia yake. Ya Mungu mengi, alipokuwa akifata kofia yake gafla aliteleza na kuangukia kwenye eneo ambapo maji yanajizungusha kwa kasi mno almaarufu 'nienga' kwa kule Unyakyusani. Alijitahidi kuogelea ili ajinasue lakini wapi, alipiga 'kantundu' yaani mbinu ya kuzama ili uinukie upande wa pili lakini nienga ilimzidi nguvu hatimaye alizama na kufa maji.
Atupele aliendelea na safari huku akiamini mwenzake atafata na alipofika nyumbani alisimulia mkasa mzima na Mama Atupele alichinja jogoo mkubwa ili jioni ya siku hiyo waende kwa akina Ndabhiti ili kushukuru kwa wema aliotendewa mtoto wao. Sasa walipokuwa njiani katika kitongoji cha Ipyana kuelekea mpakani mwa kitongoji cha Kikubha ndipo Mama Atupele na Mama Ndabhiti walipokutana. Mama Ndabhiti alikuwa anaenda kwa kina Atupele kumuulizia mwanae ambae alikuwa hajafika nyumbani mpaka jioni ya saa moja.
Kwa kawaida vijana waliokuwa wakienda msituni ilikuwa ada yao kurudi nyumbani si zaidi ya saa tisa haswa wanapokuwa wamejihimu muda wa saa kumi na moja alfajiri kwenda msituni.
Mwisho wa yote ukweli ulielezwa kwamba pamoja na uokozi aliofanya, Ndabhiti alibaki nyuma huku mwenzake akitangulia kwenda nyumbani. Wazee walijuzwa kuhusu tukio hilo na vijana nane hodari akiwemo Atupele wakaagizwa wafuatilie kuanzia pale mto Lufilyo na walipofika hapo waliona mzigo wa 'mapapati ukiwa bado upo pale pale. Walipoangaza huku na huko mdipo walipomwona Ndabhiti akiwa amekufa maji huku akielea katika 'nienga' yaani maji yanayojizungusha yenyewe.
Kulikuwa na imani kwamba katika eneo hilo kuna mashetani yanayovuta watu na kuwafanya kafara, basi mazishi yakafanyika kwa majonzi makubwa. Atupele alilia sana hadi kutokwa makamasi lakini haikusaidia. Jambo moja aliloendelea kulifanya ni kuhakikisha anawapelekea gunia mbili za mahindi na maharage wazee wa Ndabhiti na alikuwa akifanya hivyo kila mwaka.
Sasa ni juzi tu umoja wa wandishi wa habari mkoani Mbeya waliazimisha siku ya habari yaani media day. Pamoja na mambo mengine, nimefuatilia kwa umakini mkubwa kuhusu namna sherehe hizo zilivyofana na maudhui yake lakini sijashawishika kwa namna ambavyo Mwandishi Daudi Mwangosi alisahaulika. Ni kweli kwamba aliuwawa akiwa Iringa lakini nyumbani kwao ni Mbeya na ndiko alikozikwa.
Askari polisi akielekeza mtutu wa bunduki kwa mwandishi Daudi Mwangosi |
Ni dhahiri Kaka yangu Daudi Mwangosi aliuwawa akijaribu kutekeleza majukumu yake muhimu kitaaluma na kwa maslahi ya umma ya kutafuta na kuulisha umma habari kuhusiana na masuala yahusuyo demokrasia. Alikuwa akiripoti tukio la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuzindua matawi ya chama kijijini Nyororo, Iringa. Sasa twaweza jumuisha kwamba Daudi aliuwawa kwasababu watawala hawakupenda aripoti ukweli kwamba upinzani ulikuwa ukijipanga vyema na kupata nguvu au sababu nyinginezo kama zilivyotajwa na tume iliyoundwa na Jukwaa la Wahariri, Tume Teule ya Bunge au ile Tume ya Waziri wa Mambo ya Ndani.
Lengo si kurudia yaliyojadiliwa zamani bali yale ambayo ni muhimu lakini hayakujitokeza katika maadhimisho ya siku ya habari jijini Mbeya. Leo hii ukifika katika ofisi za umoja wa waandishi wa habari mkoani Geita, kwa nje tu utakutana na picha ya Daudi Mwangosi akielezwa kuwa mtetezi wa uhuru wa habari aliyeuwawa kishujaa. Inakuwaje wandishi wa Mbeya waserebuke tu na kunywa bia pasipo kufanya chochote cha kutufanya tuone wanathamini mchango wa Mwangosi.
![]() |
DAUDI MWANGOSI ENZI ZA UHAI WAKE |
Ina maana 'Mapapati' aliyokuwa akiyatafuta Mwangosi ili wandishi waelekewe nyumba zao za uhuru wa kupata habari, kuripoti na kuwajibika kwa umma hayana kazi tena?
Ni miaka karibia mitatu tangu afariki, je hawapo kina Atupele wa kumfariji Mama Daudi japo katika kila hafla ya mwaka. Yote tisa, jambo la msingi ni kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo tunahitaji watu wenye ujasiri kama wa Daudi Mwangosi. Watu wasio na woga wa kwenda kwenye mkutano wa chama chochote kile kuchukua habari muhimu kwa manufaa ya umma.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyiremba Munasa( katikati) akiwa pamoja na viongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoani mbeya (Mbeya press) Mwenyekiti Modestus Mkulu kushoto na Emanuel Lengwa Katibu,Katika sherehe ya waandishi wa habari Mkoani hapa ambayo imefanyika June 11 katika ukumbi wa JM Hotel Picha Keneth Ngelesi.
Lakini kwa mlolongo wa maadhimisho ya juzi nashawishika kuamini mambo mawili makubwa. Awali ni kwamba ule msemo wa yaliyopita si ndwele umependwa na baadhi ya wandishi wa habari jijini Mbeya na ndiyo maana hakukuwa na ujumbe wa maana sana wa kumkumbuka Daudi Mwangosi na kupeana moyo wa kuiga ujasiri ule ili kukuza demokrasia nchini ni kuzipigia chapuo haki za waandishi wa habari ikiwemo haki ya kuishi.
Waandishi wakisakata rhumba katika hafla ya Media Day |
Mwisho, ningependa kuwapongeza wandishi wa habari jijini Mbeya kwa kuadhimisha Media Day hapo juzi lakini nawakumbusha kwamba wakati ukuta, msifyate mkia na kuacha kuwakumbuka watu waliojitolea maisha yao katika kutekeleza na kutetea haki za waandishi wa habari na umma wa Watanzania.
DINI
ni taasisi ya kijamii na kwa sababu hiyo ukinzani wa kidini ni jambo la
kawaida, tangu kale hadi leo. Baadhi ya kinzani zilizotikisa jamii na
ustaarabu wake ni mbili, zote zilitokea karne ya 16 inayoitwa Enzi za
Mwamko “– Age of Enlightenment”
Na katika karne ya 20, pale wanyonge wa dunia hii walipoanza kuhoji nini nafasi ya kanisa dhidi ya maonevu ya kijamii na kiuchumi waliyotendewa wafuasi wa kanisa na wenye nguvu; kanisa, pengine kwa kuhofu ukinzani na maasi, lilianzisha dhana ya “Theolojia ya ukombozi”.
Hii ni dhana inayopinga maonevu kwa kutojikita, na kwa kazi pekee, ya kanisa ya awali ya kumwandaa mwanadamu kwa maisha mema mbinguni pekee, licha ya kuonewa na kunyanyaswa duniani; ikawa ni pamoja na kumfanya aishi maisha mema pia duniani akisubiri ufalme wa mbingu.
Hakuna mtikisiko mkubwa wa Kanisa Katoliki kama ule ulioletwa na Mfalme wa Uingereza, Henry wa Saba katika karne ya 16; na ule wa mwanazuoni Mjerumani, Dk. Martin Luther, karne hiyohiyo ambao kwa nyakati tofauti walifarakana kichwa kichwa na Kiongozi wa Kanisa hilo, Baba Mtakatifu, juu ya imani na Papa akasalimu amri.
Henry alijitenga na Kanisa Katoliki na kuanzisha Kanisa la Anglikana; wakati Luther aliasi, akaanzisha Kanisa la Kilutheri. Hawa wawili tunaweza kuwaita wababe wa imani, kwa zama hizo.
Ieleweke kuwa, ugomvi, mifarakano na ukinzani wa kidini hutokea zaidi kwenye dini zenye Katiba zilizoandikwa, yaani misahafu ya dini, kwa sababu kuu mbili: Ya kwanza ni kwa wale waliopewa mamlaka ya kusimamia Katiba ya [neno la] Mungu kujikweza na kutenda au kuagiza kufanyika mambo tofauti na yaliyo nje ya maandiko wakidai kuwa mamlaka ya kuagiza hivyo wamepewa na Mungu kwa njia ya “kupakwa mafuta”.
Sababu ya pili ni udhaifu katika kutafsiri misahafu hiyo bila kuzingatia nyakati na mazingira ya jamii inayobadilika haraka. Ni wazi kwamba, dini inayobaki nyuma ya maendeleo ya jamii kwa kushindwa kuelezea au kutatua matatizo ya jamii hiyo inayobadilika, imo hatarini kupata upinzani na uasi mkubwa kutoka kwa waumini wake.
Mifarakano ya aina hii haitokei kwa waumini wa dini ya Kikristo pekee, bali ipo kwa Waislamu pia, nayo haikuanza leo. Kwa mfano, kugawanyika kwa Waislamu katika madhehebu ya Sunni na Shia hapo kale, ni matokeo ya sababu kama hizi.
Mfalme Henry wa Nane wa Uingereza, alishika madaraka na kutawala nchi hiyo mwaka 1509, akiwa kijana mdogo tu wa miaka 18. Alikuwa kijana mbunifu, asiyejali kitu, mpenda makuu, anasa na vimwana; mchoyo na asiyependa kupingwa kwa aliloamini.
Henry alirithi mke aliyeitwa Catherine kutoka kwa marehemu kaka yake, Mfalme Henry wa VII, kama mke wa kwanza kati ya wanawake sita aliotokea kuoa baadaye kwa nyakati tofauti.
Ingawa Sheria za Kanisa Katoliki hazikuruhusu mtu kurithi mke wa mtu mwingine, lakini kwa ajili ya Henry pekee, kilitolewa kibali maalum na Papa [Papal special dispensation] kuruhusu ndoa hiyo ili kuendeleza uhusiano kati ya Uingereza na nchi ya Hispania alikotokea Catherine, binti wa Mfalme Ferdinand na Malkia Isabella wa nchi hiyo. Uingereza na Hispania zilikuwa nchi kati ya nyingi za himaya ya Ukristo [Christendom].
Baada ya miaka kadhaa, Henry VIII alianza matata na Catherine, huku akiwania kumtaliki. Sababu kubwa alizotoa ni pamoja na mama huyo kushindwa kumzalia mtoto wa kiume ambaye angerithi kiti cha Ufalme. Aliihusisha hali hiyo na laana toka kwa Mungu kwa sababu ya kukiuka maandiko ya Torati, yaliyokataza mtu kurithi mke wa nduguye kama alivyofanya yeye.
Lakini pengine hiyo ilikuwa ni kuficha ukweli, kwani alimpenda kimwana mwingine aliyeitwa Anne Boleyn na ambaye aliwania kumuoa.
Kwa kuwa Kanisa halikutambua kitu kiitwacho “talaka”, ilikuwa lazima kwanza amwombe Papa kama Mkuu wa Kanisa duniani, atoe kibali maalumu cha kumwacha mkewe Catherine. Ili kufanikisha talaka hii, Henry alimpa jukumu la kufuatilia kibali, rafiki yake mkubwa na mshauri, Kadinali Wolsey ambaye pia alikuwa Askofu Mkuu wa York; lakini alishindwa baada ya Papa kukataa katakata kutoa kibali hicho. Henry alikasirika na kumfukuza kazi Wolsey kwa kushindwa kumshawishi Papa juu ya talaka.
Kwa kuchukizwa na uamuzi wa Papa wa kukataa kumtaliki Catherine, Henry alijiengua kwenye kanisa Katoliki na akajitangaza Mkuu wa Kanisa jipya la Anglikana la Uingereza; na hapo hapo akavunja ndoa na Catherine. Kuanzia hapo Henry na kanisa lake hakumtambua Papa wala kanisa la Roma. Aliendelea kuoa wanawake wengine watano mmoja baada ya mwingine, katika maisha yake; watatu kati ya hao aliwaua baada ya kuwafumania au kuwatuhumu kwa ugoni.
Papa alijibu mapigo kwa kumtenga Henry na Kanisa kwa kuuasi mfumo wa Kikatoliki, na kwa kumuasi Kristo na Kanisa pia. Kanisa la Anglikana, aliloanzisha Mtawala wa Uingereza linaongozwa na Kiongozi huyo huyo badala ya Papa wa Roma hadi leo.
Uasi wa Mfalme Henry ulipewa nguvu na dhana kwamba Papa, kama binadamu tu, hakuwa na mamlaka kulazimisha ndoa (kati yake na Catherine) iliyokuwa kinyume na maandiko ya msahafu wa dini. Pili, Henry aliamini kwamba, katika dunia ya binadamu huru anayeongozwa na Mungu mwenye upendo, Mungu asiyejua kunyima aombwalo, ndoa lilikuwa jambo la hiari kati ya mwanaume na mwanamke. Uhuru huo ni pamoja na uhuru wa kuoana na kuachana.
Kwa kifupi, changamoto ya Mfalme Henry wa VIII dhidi ya Papa, ilikuwa juu ya uwezo wa kiongozi huyo wa Kanisa kutenda nje ya maandiko, tafsiri ya maisha ya ndoa katika jamii inayobadilika, na mantiki nzima ya uhusiano wa kimataifa (Hispania na Uingereza) kupewa umuhimu katika imani ya dini na utawala wa Kanisa. Huyo alikuwa Mfalme Henry wa VIII dhidi ya Papa.
Martin Luther kama Henry?
Pengine mtu pekee aliyeleta mtafaruku mkubwa kuliko wote katika historia ya Kanisa, akihusisha dhana zote mbili na migongano tuliyoelezea mwanzoni mwa makala ni Martin Luther, mwanazuoni, Kasisi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu. Yeye ndiye mwanzilishi wa Kanisa la Kilutheri lililopo hadi leo. Tofauti na mfarakano kati ya Mfalme Henry na Papa, uliotokana na mitazamo tofauti ya kidunia, mfarakano kati ya Martin Luther na Papa uliegemea zaidi kwenye imani, ukamilifu wa Injili na nafasi ya kanisa katika jamii.
Martin Luther alizaliwa Novemba 10, 1483 katika mji wa Eisleben, nchini Ujerumani. Akiwa na umri wa miaka 18, alijiunga na Chuo Kikuu cha Erfurt kwa masomo ya juu na kujipatia Shahada ya Pili katika sanaa (M.A) mwaka 1505. Akiwa chuoni Erfurt, siku moja, alibahatika kuona katika maktaba ya Chuo, kitabu kitakatifu kiitwacho “Biblia”, akakisoma na kushangazwa na yaliyomo.
Kabla ya hapo, waumini wote wa dini walizoea “kulishwa” neno la Mungu (Biblia) na wahubiri bila kujua yaliyoandikwa katika kitabu hicho.
Tangu karne ya 13, kanisa lilipiga marufuku waumini wa kawaida (walei) kusoma au kushika Biblia kwa hofu ya kupotosha tafsiri ya kitabu hicho. Akipiga marufuku usomaji wa Biblia mwaka 1229, Papa Gregory wa 10 alikuwa na haya ya kusema:
“Tumepiga marufuku Walei kumiliki wala kusoma nakala za Agano la Kale na Agano Jipya …. Tunakataza kabisa kabisa vitabu hivyo kutafsiriwa katika lugha za kienyeji (kutoka lugha ya Kilatini)”.
Agizo hili lilirudiwa kwa kusisitizwa tena katika Azimio la Kikao cha Maaskofu kilichofanyika mwaka 1234 mjini Taragona, Italia kwamba: “Mtu haruhusiwi kumiliki vitabu hivi viwili [Agano la Kale na Agano jipya]; na yeyote aliye navyo, avirejeshe hima kwa Askofu wa eneo lake katika muda wa siku nane tangu tarehe ya agizo hili, ili vichomwe moto”.
Mwaka 1508, Martin Luther alijipatia Shahada ya Udaktari wa Falsafa [PhD] ya Theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Wittenberg, Ujerumani ambako pia alifundisha Filosofia na wakati huohuo akiwa Kasisi.
Akiwa amesheheni nadharia za wasomi (na baadaye Watakatifu) kama vile kina Mtakatifu Augustine (354 – 430) na Thomas Aquinas (1224 – 1274), Martin Luther aliamini kwamba Biblia ndiyo Sheria Kuu ya imani ya dini ya Kikristo, na kwamba sheria zingine za binadamu zinazokinzana nayo lazima zibezwe kwa sababu sio sheria halali – “Lex esse non videbitur quae justa non “fuerit”.
Hapa Luther alikuwa anazungumzia Sheria na Kanuni za Kanisa zinazotungwa kukidhi matakwa ya binadamu na zinazopingana na au zinazotetea na kuendeleza ubinafsi wa wenye madaraka ya Kanisa. Aliamini kwamba, hakuna mtu mbadala wa Yesu duniani, na kwamba viongozi wa dini ni binadamu tu kama waumini wengine, (Luka 4:8).
Dhana hii ya Luther ilipingana na ile ya Papa Innocent wa Tatu ambayo tayari ilikuwa sehemu ya Sheria za Kanisa, iliyodai kwamba, Papa ni mwakilishi mteule wa Yesu duniani (Soma: Decretals of the Lord Pope Gregory IX).
Mwaka 1510, Martin Luther alisafiri kwa miguu kwenda Roma kuonana na Papa. Inadaiwa kuwa, ziara hii ya Roma ilimfunua macho juu ya kuvurugwa kwa misingi ya Kanisa, na jinsi viongozi wa Kanisa walivyoishi maisha ya ufahari, anasa na upondaji mali na wa jasho la waumini.
Pengine jambo lililomkera zaidi Luther hadi akaamua kuanzisha ukinzani na utawala wa Roma (Papa), ni suala la biashara ya Hati za Kitubio (Indulgences).
Nyakati hizo, Kanisa liliamini kwamba matendo mema ya Mitume na matendo matakatifu ya Yesu Kristo yalijumuishwa kuunda kile kilichoitwa “Hazina ya Matendo Mema” (Treasury of Merts) chini ya usimamizi wa Papa. Kutoka Hazina hii Papa alikuwa na uwezo wa kutoa Hati za Vitubio kwa wenye dhambi bila ya kutubu.
Ilidaiwa, hati hizo zilikuwa na uwezo wa kumwondolea dhambi au adhabu mkosaji aliyezinunua, kwa makosa yake ya nyuma, ya sasa na yajayo; na kwamba hapakuwa na sababu tena ya kutubu makosa hayo. Vivyo hivyo, ilidaiwa kuwa, Hati za Kitubio ziliweza kuwaondolea dhambi ndugu za aliyezinunua walioko toharani na wafu, wakaweza kwenda mbinguni moja kwa moja hima, mara tu fedha zinapoingia kwenye mfuko wa mkusanyaji. Kwa Luther, hili ilikuwa biashara haramu na ulaghai mkubwa kwa Mungu na Kanisa.
Mtu aliyetumwa na Papa Leo wa 10 kuuza hati hizo nchini Ujerumani, alikuwa Kasisi aliyeitwa John Tetzel. Watu wengi walizinunua lakini Luther alikataa kutambua uwezo na thamani yake.
Kama hatua ya kupinga biashara hiyo haramu ya kiroho, Novemba 1, 1517, Martin Luther aliandika pingamizi 95 za biashara hiyo ya hati za Kitubio na kuzibandika kwenye lango kuu la Kanisa la mjini Wittenberg ambalo lilikuwa makutano ya Wasomi.
Nakala za pingamizi hizo zilipelekwa kwa Papa, ambapo Wasaidizi wa Kiongozi huyo walimshauri asikoseshwe usingizi na kiburi cha Luther kwani alikuwa unyoya mmoja tu kati ya manyoya mengi.
Mmoja wao, Prieria, alijipiga kifua na kudai kuwa Papa, katika wadhifa wake kama Mkuu wa Kanisa hawezi kukosea, na kwamba nadharia zilizopitishwa na Kanisa zinawabana waumini wote, wapende wasipende, kwa kuwa yeye ni mrithi wa Yesu, na kwamba analofungua duniani linafunguliwa pia mbinguni.
Pingamizi za Martin Luther zilivuma kama moto porini na kuathiri kwa kiasi kikubwa mapato ya Kanisa kiasi kwamba Papa Leo wa 10 alilazimika kumwita Luther mjini Roma Julai 1518, kujibu mashitaka. Luther alipokataa kwenda, Papa alimtuma mwakilishi wake, Kadinali Legate Cajetan azungumze na Luther; lakini Martin hakukubali “kugeuka jiwe”.
Hatua hii, badala ya kutuliza hali, ilimwongezea Luther umaarufu nchini Ujerumani na kuamsha chuki dhidi ya Papa miongoni mwa raia na wasomi, wakidai kuwa hatua ya Papa ilikuwa ni ya kidikteta kwa lengo la kupotosha ukweli.
Katika malumbano ya ana kwa ana hadharani, kati ya Luther na Mwanazuoni mwenzake, Kasisi John Nok mjini Leipzig, yaliyodumu kuanzia Juni 27 hadi Julai 15, 1519, Martin Luther aliweza kuwashawishi watu kwamba, hakuna Sheria kuu ya Kanisa kuliko Biblia, na kwamba Sheria za Papa ni kielelezo cha uasi juu ya neno la Mungu.
Nchini Ujerumani, jina la Martin Luther lilianza kung’ara kama theluji; maandishi na hoja zake zilivuka mipaka ya nchi hadi Ufaransa, Hispania, Ubelgiji, Italia na dunia yote ya Ukristo. Aliungwa mkono na watawala wa nchi yake na hivyo kuamua kuvunja uhusiano na Roma.
Baada ya kufanikiwa kuvunja uhusiano huo, Martin Luther sasa aligeukia falsafa ya Sakramenti na kuzipunguza kutoka saba hadi tatu, kwa kubakiza Sakramenti ya Ubatizo, Sakramenti ya Kitubio na Sakramenti ya Ekaristi takatifu. Alidai, Maandiko ya Biblia yako juu ya Kanisa la Roma.
Desemba 10, 1520, Papa alimtuma Eck kumpelekea Luther Hati ya Apizo na kutengwa na Kanisa, lakini Luther aliipokea na kuichoma moto hadharani, huku akishangiliwa na umati wa watu – wanafunzi, madaktari na raia wengine. Huo ndio ulikuwa mwisho wa uhusiano wa kikanisa kati ya Ujerumani na Roma; hilo ndilo lilikuwa chimbuko, kumea na kukua kwa Kanisa la Kilutheri lililopata jina hilo kwa heshima ya (Martin) Luther.
Ni wazi kwamba, Papa hakuwa makini katika kushughulikia mgogoro huo. Kwa kushindwa kumsikiliza Luther, Papa Leo alijikosesha njia, hasa alipotanguliza Ukuu wa Kipapa (Papal Supremacy) katika hali tete iliyoonyesha kila dalili za Kanisa kuchechemea nyuma ya wakati na kupelekea maasi yaliyotokea.
Hatuwezi kusema kwamba Martin Luther alikuwa muasi bila uhalali, bali kwamba alikuwa mwanaharakati aliyeitumia vema elimu yake ya theolojia kutetea Katiba ya Imani ya dini yake ambayo ilikuwa hatarini kupotoshwa na sheria za binadamu.
Leo mambo mengi aliyotetea Martin Luther nyakati zake yanatekelezwa na Kanisa Katoliki la Roma, kuonyesha kwamba hakuwa hayawani bali alikuwa sahihi kwa kutenda alivyofanya.
Haya ni pamoja na sisitizo jipya juu ya umuhimu wa kufuata maandiko matakatifu katika maisha na mafundisho ya Kanisa (Constitution on divine Revelation).
Pia leo, msimamo wa Kanisa uko wazi kwa watu wote juu ya umuhimu wa Kanisa hilo kujipeleleza ili liendane na wakati [Constitution on the Church, 8, Decree on Ecumenism]. Hivi leo, Kanisa linajiona kama sehemu ya jamii inayoishi, linaielewa jamii lilimo na dhana nzima ya dhambi. Ndiyo maana limeanzisha “Theolojia ya Ukombozi” [Liberation Theology], ambapo hapo nyuma hii ingeitwa itikadi ya Ki-Karl Marx [Mjerumani] au Ukomunisti.
Sisitizo sasa ni kwamba, uchungaji si madaraka, utukufu wala utajiri, bali ni huduma [Decree on the life and Ministry of Priests]; nafasi sawa ya uchungaji kwa waumini wote – kila muumini ni mchungaji kwa haki yake [Decree on the Apostolate of the Laity].
Mwisho, kutafsiriwa kwa Biblia katika lugha mbali mbali za kienyeji ni ushindi kwa Luther dhidi ya Sheria za Kanisa la kale.
Kuna mantiki katika maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, alivyoandika katika kitabu chake – “Binadamu na Maendeleo”. Kwamba: “……. Ikiwa [waumini] hatutashiriki kwa vitendo katika kuondoa utaratibu wa maisha na wa uchumi unaowadidimiza watu kwenye umasikini, uonevu na unyonge, basi Kanisa [dini] litakuwa halina uhusiano na maisha ya binadamu, na dini itakuwa kama ni mkusanyiko wa imani za ushirikina zinazokubaliwa na wenye hofu tu ……. Na ikiwa itakuwa hivyo, Kanisa litakufa [litasambaratika], maana litakuwa halina maana inayoeleweka kwa mtu wa kisasa”.
Kwa migogoro ya kidini inayozuka mara kwa mara, je, tutarajie kuibuka kwa akina Martin Luther wa enzi zetu?. - See more at: http://www.raiamwema.co.tz/wababe-wa-dini-waliotikisa-kanisa-katoliki#sthash.Z8CuWquR.dpuf

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni