
Watu 2 wameuawa Burundi katika
mashambulizi ya gruneti na ufyatulianaji risasi katika ngome za upinzani
katika mji mkuu wa Bujumbura siku moja kabla ya uchaguzi wa wabunge.
Uchaguzi
huo ambao umekumbwa na utata baada ya makundi ya upinzani kuandamana na
ilikupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.Upinzani unadai kuwa rais Nkurunziza anakiuka katiba ya taifa na mapatano ya Arusha yalyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Walioshuhudia mauaji hayo wanawalaumu polisi kwa mashambulizi na vifo hivyo vilivyotokea katika maeneo ya mji mkuu wa Bujumbura ambayo yanadhaniwa kuwa ni ngome ya vyama vya upinzani.
Jumamosi watu waliokuwa wamejihami na bunduki walivamia kituo cha kuhifadhia makaratasi ya kupigia kura na kuyachoma moto.

Upinzani umekuwa ukiandaa maandamano mjini Bujumbura ilikumshinikiza ajiondoe katika kinyang'anyiro hicho.
CHANZO:BBC SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni