Lebo

Jumatano, 17 Juni 2015

Askari wa jeshi la polisi ni wanachama wa CCM?

Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Kinana akipanda boda boda ya askari polisi
 Ukitazama vema hiyo picha hapo juu utakuwa na machaguo mawili, aidha askari anayemwendesha Katibu Mkuu wa CCM, Mhe.Abdullahman Kinana hajui mipaka yake ya kazi au Katibu Mkuu wa CCM amemshurutisha askari huyo kufanya hivyo kwa maslahi ya chama chake au ubabe tu wa wenye mamlaka nchini Tanzania. Mtoa taarifa wangu amesema "imekuwa kawaida kwa Katibu Mkuu wa CCM kujinasibisha kwa watu wa hali ya chini lakini hapo amevuka mipaka".

Ni kweli mara kadhaa Mhe.Kinana ameonekana runingani akichezea matope sawa na waashi, amewahi kuonekana kwenye mashamba ya chai akiigiza kuchuma chai n.k lakini hapo alipofika kwa askari wetu wanaolipwa kodi za wananchi wa vyama vyote halafu anajengewa taswira kuwa mwanachama wa CCM, hii haivumiliki.
Ni mara nyingi jeshi la polisi limetuhumiwa na vyama vya upinzani kwamba linakipendelea chama tawala, tuhuma zimekanushwa  mara nyingi lakini kwa hiki kitendo cha Mhe. Kinana lazima kikemewe. Ni vigumu kuamini kwamba askari huyo pichani hakufunzwa kwamba hastahili kuwa shabiki wa chama chochote, wala asishiriki siasa zaidi ya kupiga kura tu?

Hivi Mhe.Kinana anataka tuamini kwamba hajui waraka namba 1 wa mkuu wa utumishi wa umma unasema nini kuhusu watumishi wa umma kutokushiriki siasa? Ngoja nimkumbushe yeye na watumishi wengine wa umma sambamba na wanasiasa wanaopenda sifa zisizostahili sambamba na siasa zinazoweza kuchochea ghasia.



JAMHURl  YA MUUNGANO   WA TANZANIA


OFISI  VA RAIS IKULU,
S.L.P  9120,
DAR-ES-SALAAM. Kumb. Na. SHCIC.180/2/113                                        26 Juni,  2000
WARAKA   WA MKUU   WA UTUMISHI    WA UMMA
NA.  1 'WA MWAKA   2000


KUHUSU  MAADILI  YA WATUMISHI  WA UMMA  KATlKA MFUMO  WA VYAMA  VINGI  VYA SIASA

1.0   UTANGULIZI:


1.1    Kuanzia  mwaka  1965 hadi  1992 Tanzania  ilipokuwa  na Mfumo wa  Siasa  wa  Chama  Kimoja   Watumishi   wote  wa  Serikali  na Vyombo  vyake  siyo tu waliruhusiwa   bali  ilionekana   ni wajibu wao  kushiriki   katika  mambo   ya  kisiasa.     Shughuli   nyingi  za kiserikali  na za kisiasa zilikwenda  kwa pamoj ana palikuwepo  na maingiliano  makubwa  kati ya sehemu  hizi mbili katika  shughuli zote za kiutendaji,  kiuongozi  na kiitikadi.

1.2   Kufuatia  mabadiliko  ya Katiba  ya Jamhuri  ya Muungano  wa Tan- zania yaliyofanyika   Julai,  1992 na kuruhusu  mfumo  wa vyama vingi  vya  siasa,  Serikali   ilitoa  maelekezo   ya jinsi  watumishi watakavyoshiriki  katika mambo yaSiasa  kupitia Waraka wa Mkuu wa Utumishi  wa Umma  Na.  1 wa Mwaka   1992.



1

2.0   UTARATIBU     ULIOTOLEWA     KATlKA    WARAKA   WA MKUU  WA UTUMISHI WA UMMANA.1  WAMWAKA  1992:

Utaratibu  uliotolewa   katika  Waraka  wa Mkuu  wa Utumishi   wa Umma  Na.  1 wa Mwaka   1992 uliwagawa   watumishi   wa umma katika    makundi     mawili    na   kuweka     Masharti     ya   namna watakavyoshiriki   katika  Siasa.

2.1  Watumishi  wa Kundi  "A" walijumuisha   Watumishi  wa ngazi zajuu Serikalini,       Serikali   za  Mitaa   na  katika   Mashirika    ya  Umma wanaoshughulikia       uandaaji   11a usimamizi    wa  sera.    Hawa  ni watumishi   waandamizi     wenye   Madaraka    kuanzia    ngazi   ya Mkurugenzi  na kuendelea  juu, Meneja  Msaidizi  na kuendelea  juu na ngazi ya Mkurugenzi  Mtendaji.

Nikienda moja kwa moja kwenye kifungu lengwa:
3.3  Mbali ya makundi yaliyotajwa katika aya ya 2 hapa juu kuna makundi ya watumishi  wa umma ambao hawakuorodheshwa    katika Waraka huo  lakini  kwa mujibu  wa Katiba  ya Iamhuri   ya Muungano   wa Tanzania, hawaruhusiwi  kuwa wanachama  wa chama choehote eha siasa  wala   kujihusisha   na shughuli  zozote  za kisiasa  isipokuwa kupiga  kura tu. Watumishi  hao ni:-

3.3.1  Askari  wa Ieshi la Wanachi  wa Tanzania  (JWTZ)  na Ieshi la Kujenga  Taifa (JKT),  Polisi na Magereza  (kwa mujibu  wa Ibara ya 147(3) na (4) ya Katiba  ya Iamhuri  ya Muungano wa Tanzania).

3.3.2   Majaji  na Mahakimu  wa ngazi  zote (kwa mujibu  wa Ibara ya  1l3A)  ya Katiba  ya Jamhuri  ya Muungano   wa Tanza- nia).

3.3.3   Wajumbe  na Watumishi  wa Tume ya Uchaguzi  na Wasima- mizi wa Uehaguzi  (kwamujibu   wa Ibara ya 74(14)na(l5)
ya Katiba  ya Iamhuri  ya Muungano   wa Tanzania).

3

3.4  Mbali ya makundi yaliyoorodheshwa  katika Katiba kutoshiriki katika siasa yapo makundi mengine  ambayo kwa mujibu wa kazi zao hayapaswi  kushiriki  katika siasa, lakini hayakutajwa  katika Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na.1 wa Mwaka  1992, mathalani, watumishi wa Idara ya U salama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia Rushwa, Msajili  wa  Vyama  vya  Siasa,  watumishi   wa  Ofisi  ya Bunge,  na Mawakili  wa Serikali.


HITIMISHO, NI WAJIBU WA WAPENDA DEMOKRASIA NA AMANI KUKOSOA PALE WENYE MAMLAKA WANAPOPOTOKA.

Mwaka 2013, Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema alipiga picha na mtu aliyevalia sare ya JWTZ katika mkutano wa hadhara na ikawa kesi kubwa mtaani. Basi sheria na iwe msumeno.

@LUMULINEWS.BLOGSPOT.COM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni