Miss Tanzania mwaka 2006 na mwigizaji wa filamu, Wema Abraham Sepetu jana June 16 kupitia kipindi cha Ala za Roho ya Clouds FM alifunguka kuhusiana na nia yake ya kuchukua fomu ya ubunge wa viti maalumu mkoani Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na Diva Loveness wa Ala za Roho jana usiku, Wema Sepetu ambaye pia ni ex-girlfriend wa mwanamuziki Diamond Platnumz alisema:
”Sasa hivi niko singida kwenye maandalizi ya kuchukua fomu kwasababu nagombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa singida, kwa hiyo nimekuja huku kuja katika kuhamasisha vijana wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura.
"Nimekuja kujiandikisha huku kwa sababu mama yangu ni mtu wa singida so nimejiandikisha tayari tukutane 15 tena kuja kuchukua fomu kwasababu fomu zinatoka tarehe 14 mwezi wa saba so inshallah tuombe uzima, kampeni zimeshaanza zile ndogo ndogo nashukuru Mungu naendelea vizuri nahitaji support kwa jamii"

Kutokana na maelezo hayo, Diva alimuuliza Wema Sepetu kuhusiana na aina ya harakati zake:
“…I Know about kampeni za chini chini ambazo ulikuwa unafanya kwa muda mrefu kwaajili ya kugombea Ubunge na umepiga picha kwa Raqay tayari ukiwa na mavazi ya CCM si ndio kampeni pale iko pale pale au??…”

Majibu Ya Wema Sepetu:
“…. Yes nimefanya so ama nilikuwa nazungumza na management yangu ambayo yupo Martin kadinda na pia yuko Petiman ambaye yupo katika suala zima la kampeni yangu.
"Watanzania wajue tu yes nitachukua fomu ya kugombea Ubunge wa viti maalumu ya mkoani Singida and tutaona uko mbele itakavyokuwa kwasababu hiki ni kinyang’anyiro naingia, ni kama vile naingia kwenye mapambano yaani vitaani so kuna kupata na kukosa ."
Diva alihoji tena, 'vipi ukikosa' "Sifikirii kukosa kwasababu mtu ukifikiri kukosa unajiweka kwenye negative side."
Kitendo cha wema sepetu si cha kwanza kwa wasanii wa bongo movie kujiingiza katika siasa, ikumbukwe kuwa hata marehemu Steven Kanumba (R.I.P) aliwahi kutangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini kabla ya kifo chake. Huu ndiyo mwaka 2015, yetu macho na tusubiri tuone.

@LUMULINEWS.BLOGSPOT.COM
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni