Lebo

Ijumaa, 12 Juni 2015

EXCLUSIVE...Profesa Ibrahimu Lipumba kuzindua safari ya UKAWA jumapili

Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA Profesa Ibrahimu Lipumba, ametangaza rasmi kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia UKAWA huku akiwa ni mtu wa kwanza kabisa katika umoja huo. Profesa Lipumba, endapo atapitishwa na wana UKAWA kugombea nafasi hiyo, basi hiyo itakuwa ni mara ya nne mfululizo kwa nguli huyo kujitosa katika mbio za urais tangu mwaka 2000,2005 na 2010.

Mwenyekiti wa CUF ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Prof.Ibrahim Lipumba


Akizungumza jana,Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo alisema, Profesa Lipumba ndiye mgombea pekee wa urais aliyetangaza nia ya kuwania nafasi hiyo.
 
Alisema muda wa kutangaza nia kwa wagombea urais kupitia chama hicho ulianza Mei 10 hadi Juni 10, mwaka huu.
 
“Kalenda yetu inaonyesha muda wa mwisho wa kutangaza nia ilikuwa juzi na aliyefanya hivyo ni Profesa Lipumba pekee yake,” alisema.
 
Alisema muda wa kuchukua fomu kwa nafasi ya urais kupitia chama hicho ulianza jana na utakamika Juni 14, mwaka huu.
 
“Mkutano huo utakaoonyeshwa moja kwa moja kupitia runinga,” alisema.
 
Mketo alisema vikao vya Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho vitaanza Julai 11 hadi Julai 12, mwaka huu ili kumpitisha mgombea urais, wabunge na madiwani.
 
“Wagombea watakaopitishwa na Baraza watasubiri vikao vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitakavyotoa mgombea mmoja katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani,” alisema. 
 
Kama Ukawa itamteua Profesa Lipumba ambaye kitaalamu ni mchumi itakuwa ni mara ya tano kuwania nafasi ya urais.
 
Akizungumzia nafasi za ubunge, Mketo alisema kati ya majimbo 189 ya Tanzania Bara, wamepata wagombea kwenye majimbo 133.
 
Alisema majimbo 56 bado hayajapata wagombea na kuwataka wafuasi wa chama hicho wenye sifa kuwania. 
 
 
Pamoja na hayo, wadadisi wa mambo ya siasa za mvumo wanaona ya kwamba kuna nguvu kubwa inayoweza kuwainua UKAWA mwaka huu endapo watakuwa kitu kimoja katika kufanya maamuzi ya nani apeperushe bendera ya umoja huo. Wapo wanaopendekeza kuwa endapo Dr.Willibrod Slaa atagombea urais huku Prof.Lipumba akiwa mgombea mwenza basi huo utakuwa mwanzo wa Tanzania mpya ambayo Mhe. Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi aweza kuwa waziri mkuu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni