Lebo

Jumamosi, 13 Juni 2015

Interpol wasitisha ushirikiano na FIFA, kisa rushwa na ufisadi

Shirika la polisi wa kimataifa Interpol limesema linasimamisha uhusiano wake na FIFA uliokuwa na lengo la kuchunguza na kukabiliana na visa vya upangwaji wa matokeo ya mechi za kandanda, kutokana na kashfa ya rushwa inayolizonga shirikisho hilo la soka duniani. 

Miaka minne iliyopita FIFA iliipa interpol dolla millioni 22 kufadhili mradi ulio na lengo la kuendeleza maadili katika secta ya michezo.Interpol inasema washirika wake wote ni sharti wadumishe na kuendeleze maadili na taratibu zinazotumiwa na interpol katika utendaji kazi wake.

A FIFA logo sits on a flag at the FIFA headquarters

FIFA imesema imesikitishwa na uamuzi huo wa Interpol na kuongeza kuwa mradi huo wa mikakati ya kuzua udandanyifu katika soka hauhusiani kwa vyovyote vile na kashfa ya madai ya rushwa dhidi ya FIFA.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la BBC, Interpol imechukizwa na mwenendo mbovu wa shirikisho la soka duniani FIFA haswa kukithiri kwa rushwa na ufisadi ndani ya Shirikisho. Katibu Mkuu Mtendaji wa shirika la kimataifa la polisi (Interpol), Jenerali Juergen Stock amenukuliwa na vyombo vya habari akisema huwezi kupinga rushwa wakati nawe ni mmoja kati ya wala rushwa. Jenerali Stock anatajwa kuwa mtendaji wa Interpol mwenye msimamo thabiti katika maamuzi yake ukilinganisha na waliomtangulia katika wadhifa huo.

Wiki mbili zilizopita, FIFA iligubikwa na kashfa lukuki za maofisa wake kujihusisha na mambo ya rushwa na kukamatwa na maofisa wa usalama wa Marekani FBI. Pamoja na mambo mengine, kashfa hizo zilipelekea kujiuzulu kwa aliyekuwa Rais wa FIFA ndugu Sepp Blatter.

Jambo hili limetafsiriwa kuwa pigo kubwa kwa wapenda soka duniani haswa wale wapenda haki na weledi katika soka, hii ni kwasababu FIFA haina chombo chake binafsi cha kiusalama kwa ajili ya kudhibiti rushwa michezoni lakini wengi wanabaki na matumaini kwamba pengine rais mpya atakaye chaguliwa hivi karibuni atarejesha hali ya amani kunako shirikisho la soka duniani hivyo Interpol waweza badili maamuzi siku za usoni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni