Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na jarida la Nairobi News, kijana Mathew Kinuthia Maina alikamatwa na maofisa usalama katika ikulu ya Kenya juni 19, 2015 baada ya kuruka ukuta na kujipenyeza ndani ya sehemu nyeti kabisa ya taifa la Kenya licha ya kuwapo ulinzi mkali wa watu na mifumo ya kielektroniki.
Baada ya kuletwa mbele ya mahakama mnamo tarehe 22 juni, 2015 kijana Mathew Maina alikiri kuruka ukuta wa ikulu ya na kutanabaisha kwamba hakuwa na lengo baya la kigaidi kama zilivyoeleza hisia za wana usalama waliomkamata. Alieleza Mathew;
Kijana maina 'MWANAMUZIKI' alitaka kumwona Rais Uhuru Kenyatta kusudi aombe msaada wa kupatiwa fedha kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake ili baadaye apate kumudu kulipa ada akirudi shule. Mpaka sasa kijana Mathew anashikiliwa na maofisa usalama wanaojishughulisha na uchunguzi wa masuala ya kigaidi. Ikumbukwe kwamba Kenya imekuwa katika hali tete kiusalama kutokana na mashumbulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na kikundi cha kigaidi cha Alshabaab.Macho na masikio ya Wakenya na wana Afrika Mashariki kwa ujumla ni kuisubiri ripoti ya polisi. Lakini yeye binafsi amesisitiza kwamba bado angali anahitaji msaada kutoka kwa Rais Kenyatta licha ya baadhi ya wanamuziki wakubwa kujitokeza kumsaidia kijana huyo ili apate kurekodi muziki wake.Kijana alikuwa na ndoto nzuri lakini alikosea njia ya kuitekeleza ndoto yake. Wadadisi wa mambo wanasema ni hali ya kawaida pale ambapo binadamu anakuwa anahitaji msaada lakini anakuwa hajui ataupata vipi. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni