 |
Ombeni Sanga |
Watu wanaposema Tanzania ina vipaji siyo vya kucheza viduku tu, kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa katika gazeti la Mwananchi la leo, kuna taarifa kuhusu kijana Ombeni Sanga aliyebuni kifaa maalumu cha kutatua tatizo la upungufu wa walimu Tanzania. Taarifa kamili iko hapa:
Alipojiunga na Shule ya Sekondari
ya Lumuli iliyopo mkoani Iringa, Ombeni Sanga alikuwa na matarajio
makubwa ya kusoma masomo ya sayansi, ili baadaye aje kuwa mvumbuzi.
Kinyume na matarajio yake, hakuweza kupata kile
alichokitarajia, kwani alikumbana na uhaba wa walimu wa sayansi shuleni
hapo jambo lililomfanya akate tamaa ya kuendelea na masomo.
“Niliamua kukatisha masomo nikiwa kidato cha
pili kwa sababu tulikuwa hatusomi masomo ya sayansi. Nia yangu ilikuwa
kuhamia shule nyingine lakini nikakosa kwa sababu sikuwa na fedha,”
anasema
Changamoto hizo zilimpa Sanga fursa ya kuwa
mbunifu na akaamua kuunda chombo alichokibatiza jina la ‘ Boxpedia’
ambacho kitatumiwa na wanafunzi kujisomea mada mbalimbali za kitaaluma
hata wakiwa nyumbani.
“Hiki kifaa kitatumiwa na wanafunzi popote pale, kitakuwa na
sauti za walimu ambao wanazichambua mada mbalimbali za masomo yote kwa
ufasaha,” anasema.
Sanga anaeleza kuwa lengo kubwa la kuunda boksi
hilo ni kupambana na na uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi. Kwake
ubunifu huo ni mbadala utakaowarahisishia kazi wanafunzi.
Hata hivyo, anasema kasha hilo halitakuwa na sauti za walimu wa masomo
ya sayansi tu bali hata masomo ya sanaa na biashara, hivyo mwanafunzi
atakuwa na uwezo wa kuchagua mada aitakayo. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
“Ni nyepesi kutumia na haina ugumu kwa sababu mwanafunzi ana
kazi ya kusikiliza tu na akitaka anaweza kuchukua taarifa muhimu kwa
ajili ya kujielewesha kwa kina mwenyewe,” anasema .
Linafanyaje kazi?
Sanga anasema boksi hilo hurekodi sauti za walimu mahiri wa masomo yote katika mada zote.
‘’Mtumiaji wa boxpedia hubonyeza ‘code’ ya mada
anayoitaka na kuanza kusikia sauti ya mwalimu wa mada katika somo kama
Baiolojia, Fizikia, historia, Jiografia au lugha,’’ anaeleza.
Anasema sauti za walimu hao zitahaririwa kwanza
kabla ya kuingizwa katika boksi hilo, kwa ajili ya matumizi na baada ya
hapo ‘code’ za kuchagua mada zitatengenezwa.
| | | | |
|
|
|
|
|
| |
|
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni