Profesa Lipumba amechukua fomu ya kugombea urais na kuahidi neema
 |
Prof.Ibrahimu Lipumba |
Mwenyekiti wa chama cha wananchi-CUF ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ametangaza nia rasmi na kuchukua fomu ya kugombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mara ya tano mfululizo.
Pamoja na mambo mengine, mambo makubwa aliyoyazungumza Profesa Lipumba ni haya hapa:
Nachukua fomu kwa mara ya tano kwa sababu;
1. Kuhakikisha tunapata Katiba mpya. Hili jina la (UKAWA)Umoja wa Katiba ya Wananchi mimi ndo nlilibuni. UKAWA ni ummoja wa vyama vilivyo sajiliwa.
2.Nina uwezo na nia ya kuwaondosha hawa mafisadi ambao badala ya
kua jela wanachukua fomu ya kugombea urais wa CCM. Wanahitajika kuwa
jela na mali zao zirejeshwe
Kidato cha tano nilisoma masomo ya hesabu uchumi na Geografia. Na chuo
niliweka rekodi ya kufaulu Vizuri ambapo chuo kiliniomba nibakie shuleni
nafundisha.
Nilienda Marekani kusoma na Kurudi kufundisha chuo kikuu cha Dar. Nilikua mshauri wa Mwinyi katika maswala ya Uchumi
Nilichaguliwa kuwa mshauri wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa katika maswala ya uchumi.
Bunge la marekani walinikaribisha niwafunde kwanini nataka madeni ya Afrika yafutwe.
Bunge la Marekani lilinikaribisha kuwashauri kuhusu mahusiano kati ya
shirika la fedha na Afrika. Ushauri ulikubaliwa. Nimefanya ushauri wa
Wizara ya fedha Namibia, Swaziland, Uganda. Katika maswala ya Ushauri
nmefanya kwa muda mrefu.
Unapozungumzia maswala ya Uchumi nayaelewa sana.
Umasikini wa Tanzania unasababishwa na Siasa mbovu za Seikali ya CCM.
Niliulizwa umeoa? Ninaye mmoja ambaye anafanya kazi Umoja wa
Mataifa ambapo yeye haruhusiwi kufanya shughuli za Kisiasa. Hata hivyo
mimi ndo nagombea urais sio familia ndio inayogombea. Kama anataka siasa
aingie kwa uwezo wake siyo aingie kwenye ubawa wa mume au mke.
Tunahitaji wakina mama waingie kwenye siasa kwa uwezo wao sio kwa kofia
za familia kama ngazi. Hata Nyerere kwenye shughuli kubwa ulikua
humuoni Mama Maria. Lakini sasa hivi wanabeba na familia zao.
3. Nataka wakina mama na Watoto wapate lisha bora na huduma za Msingi za Uzazi
kwa kila Mtanzania. Watoto wanazaa wakiwa watoto, watoto wamedumaa,
watoto wapewe Fursa za kusoma. Jambo la kuwekeza kwa watoto ndilo la msingi
Imara
4. Kumaliza tatizo la ajira. Jiografia yetu ni nzuri ambayo
ninzuri katika kujenga ajira. Mtwara kuna badari asilia ya kina kirefu.
Hapo kuna fursa ya Biashara kwani kuna gesi, Tanga kuna bandari na
kunakubali kila aina ya mazao. Vilevile sekta ya kilimo ni sehemu nzuri
sana ya kutengeneza ajira.
Ujenzi wa miundo mbinu imara, sio tu tunaongeza ajira bali usalama pia
kwani nchi nane tulizopakana nazo zinategemea bandari za Tanzania.
5. Hali ya Afya. Tunatakiwa tuwe na hifadhi ya jamii kwani wazee wanateseka kwa kuwa hakuna huduma.
6. Ufisadi. Kama nikichaguliwa kupeperusha bendera ya UKAWA, sitakuwa na huruma na mafisadi
Kama UKAWA watanipendekeza kupeperusha bendera, Nikiwa rais nitaunda Serikali ya Umoja wa kitaifa kupambana na ufisadi.
Nipo tayari Kumuunga mkono na Kumpigia debe Mgombea yoyote ambaye atapitishwa ndani ya UKAWA.
Ninacho waomba wananchi, Nendeni kujiandikisha ili tupige kura na
kulinda kura pia, kwani miaka ya kuchakachuliwa imeshapitwa na wakati.
Asanteni sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni