Lebo

Jumatatu, 15 Juni 2015

Rais wa Sudan Kaskazini Omar El Bashir atoroka Afrika Kusini

                             Rais Omar El Bashir, aliyevaa miwani na suti katikati

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa mitandaoni na katika chombo cha habari cha kimataifa- Aljazeera, ndege ya Rais Bashir iliondoka Afrika ya Kusini wakati ambao mahakama ya juu ya nchi hiyo ikiwa inajadili iwapo ni haki kisheria kumkamata Rais Omar El Bashir ili kutekeleza wito uliotolewa na viomgozi wa International Criminal Court (ICC).

Rais Omar El Bashir anashutumiwa na ICC kwa uhalifu wa kivita na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika jimbo la Khartoum, nchini Sudan.

Taarifa za Rais Bashir kutoroka nchini Afrika ya kusini zimetolewa na waziri wa habari wa Sudan ya Kaskazini. Waziri Ahmed Bilal Osman amesema kuwa serikali ya Afrika ya Kusini ilikula kiapo cha kutokumkamata Rais Omar El Bashir tangu akiwa nchini mwake pale alipoalikwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Afrika.

Awali Shirika la utangazaji la Africa ya Kusini (SABC) lilitangaza mapema leo saa nne asubuhi kwamba Rais Bashir ameondoka akisafiri na ndege yenye uwezo wa kupita majini kabla ya kupaa (Waterproof Air Force Base) katika ukanda wa Pretoria.

Lakini mwanasheria aliyesimama kwa niaba ya serikali ya Afrika ya Kusini katika mahakama kuu mjini Pretoria, alielezea mahakama kwamba Rais Omar El Bashir hakuwa mmoja kati ya watu walio ondoka na ndege hiyo.

 Mapema asubuhi ya leo, waziri wa habari wa Sudan ya Kaskazini aliliambia alinena na vyombo vya habari akisema, " Rais atarudi nyumbani ndani ya saa moja au mawili, haijalishi kama mahakama ya Afrika ya Kusini itasema polisi wa nchi wa nchi hiyo wanayo mamlaka ya kumkamata au lah, atarudi nyumbani".

Mwakilishi la shirika la habari la ALJAZEERA, Fahmida Miller ameripoti kutoka Johannesburg akisema ndege ya Rais Omar El Bashir iliondolewa uwanjani hapo na kupelekwa katika ngome ya jeshi. Na kwa kuwa jeshi halikuwa sehemu ya kesi hiyo, basi si ajabu Rais Bashir ameondoka Afrika ya Kusini kupitia moja ya kambi ya jeshi ya nchi hiyo.

KWA NINI RAIS OMAR EL BASHIR ALIWEKWA KIZUIZINI NA BAADAYE TAARIFA ZA KUKAMATWA ZIKASAMBAA MITANDAONI?

Rais Omar El Bashir anatuhumiwa kwa jinai ya uhalifu wa kivita na matumizi makubwa ya nguvu za kijeshi katika vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan katika jimbo la Khartoum.

Kwa mara ya kwanza hati ya kukamatwa kwa Rais Omar El Bashir ilitolewa mnamo mwaka 2009 lakini Rais Bashir alizikana tuhuma hizo. Akizungumza na wandishi wa habari leo jumatatu mjini Geneva, Uswisi; Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amesema sharti mamlaka ya ICC yaheshimiwe.

Wadadisi wa mambo ya kidiplomasia na uwajibikaji wa kitaasisi katika nyanja ya kimataifa wanaeleza kuwa huenda wizara ya mambo ya ndani ya Afrika Kusini ikawajibika kwa uzembe wa kumtorosha mtuhumiwa haswa endapo mahakama itathibitisha kuwa Rais Bashir alistahili akamatwe.

 NINI MAONI YAKO? 

 

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni