Lebo

Jumatatu, 15 Juni 2015

Tanzia: Kiongozi Mkuu wa Waislamu afariki dunia

 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTIo4LOIZla4xn5Tnv49UaMeMhht9R2_4pZlkppqsQXVr8q4djZ-Q9FssO4q0rjWOr2YwHu0Osj4eYgWqjnXiZCmkpN6X0kA-DcjoexjWqQs2s_rjGeauCdkybNJoaq7GFiV4GVzF-hRE/s1600/GO9G3989.JPG
Mufti Simba (enzi za uhai wake) akisalimiana na Rais Kikwete.Hapa ilikuwa mwaka 2011

Kiongozi Mkuu wa Waislamu nchini Tanzania, Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki dunia leo asubuhi akiwa Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari pamoja na shinikizo la damu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN
Taarifa za awali zinaeleza kuwa mwili wa marehemu utaagwa rasmi Dar es salaam siku ya kesho na baadaye mipango ya kuusafirisha mwili kwa ajili ya mazishi itafanyika.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa mkoani Shinyanga, nyumbani kwake endapo ratiba ya taarifa iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Dar es salaam haitabadilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni