![]() | ||||
Wanasayansi nchini Uingereza
wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu
kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.
Watafiti
katika chuo kikuu cha Sheffield kwa siri walichukua filamu ya watoto wa
umri wa miaka sita na saba wakifanya mtihani uliokuwa na majibu ambayo
yalikuwa yameandikwa nyuma ya zao.Wale waliodanganya kuhusu kile waliochofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao kukumbuka walichofunzwa. Mmoja ya watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uwongo. Utafiti huo ambao pia umechapishwa katika jarida la Journal of Experimental Child Psychology umetanabaisha kwamba ni vema kuwa namna katika namna ya kuchukua hatua dhidi ya watoto wadanganyifu maana kama tabia yao ya udanganyifu itabadilishwa kisaikolojia kwenda kwenye ukweli waweza kuwa watu makini na wenye mafanikio makubwa. Akifafanua kwa kina kuhusu utafiti huo, Elena Hoicka kutoka katika kitengo cha idara ya saikolojia cha chuo kikuu cha Sheffield amesema, "Wakati wazazi wengi hawapendezwi na vitendo vya watoto wao kuwa wadanganyifu, angalau watatulizwa wakisikia kwamba kuna faida kwa watoto wao kudanganya. Hii itamaanisha kwamba watoto wao wamekuwa a uwezo mzuri wa kufikiri na kutunza kumbukumbu" Dr.Elena ameelezea pia kuhusu utafiti mpya wanaopanga kuufanya kw kuangalia dhima kuu tatu ambazo zitaangazia namna ambavyo watoto wanajifunza kudanganya kwa kuangalia masuala haya: 1/ Udanganyifu ni ujuzi muhimu kijamii kwa watoto wadogo. 2/Kuwadanganya watoto wako, kunaweza kuwa sababu ya wao kutokukuamini. 3/Watoto wadanganyifu wana nafasi kubwa ya kukua na kuwa raia wema". Katika utafiti huo, watoto wenye umri kati ya miaka 6 na 7 walipewa zoezi la kutafuta majibu ya kadi walizopewa kwa kucheza game maalumu. Watoto waliotazamia majibu kwa kugeuza kadi walizopewa huku wakirekodiwa na camera iliyofichwa walidanganya kwamba hawakutazamia. Kikubwa zaidi ni kwamba watoto hao walifanya vizuri katika mtoto uliofuatia kuhusu utunzaji kumbukumbu. Sasa ni kazi kwenu wazazi na walezi kuhusu namna ya kuwalea watoto wadanganyifu, naamini hata watangaza nia ya kwenda ikulu ya Tanzania waweza kuinyaka hii na kupendekeza kwamba somo la UDANGANYIFU liingizwe kwenye mitaala ya shule za msingi. Kama una maoni kuhusiana na habari hii usiache kuniandikia. Enjoy with:lumulinews.blogspot.com |
Jumamosi, 20 Juni 2015
Utafiti:Watoto waongo ni werevu kuliko wakweli
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni