Baada ya maneno mengi kuibuka mitaani kuhusu hatua ya wabunge kulipwa kiinua mgongo cha milioni 230 tsh wakati hali ya uchumi miongoni mwa wananchi walio wengi, Mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mhe.Tundu Lissu ameandika waraka ufuatao akijibu kwa ujumla wake kuhusu fedha hizo:
"Habari za wakati huu kila mmoja na heshima inayomstahili. Jana usiku niliahidi kutoa maelezo na msimamo wangu juu ya suala la kiinua mgongo cha wabunge tunachosikia tutalipwa mara baada ya kumaliza Bunge wiki ijayo.
Nasema 'tunachosikia tutalipwa' kwa sababu hadi sasa hatujapewa taarifa rasmi juu ya kiasi tutakacholipwa. Jambo la kwanza, sio sisi wabunge tunaoamua tulipwe kiasi gani cha mshahara na posho mbali mbali.
Kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji Bunge, ni Rais Kikwete ndiye anayeamua masuala haya, baada ya kushauriwa na Tume ya Utumishi wa Bunge.
Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa imeweka masharti ya kiinua mgongo cha 40% ya mishahara yote. Posho nyingine tunazosikia tutazilipwa zitakuwa zimetokana na Sheria ya Uendeshaji Bunge. Ninafikiri hivyo kwa sababu sijaona taarifa yoyote rasmi juu ya jambo hili. Je, nitazichukua??? Ndiyo!!!!
Kwanza, kwa sababu nazihitaji kwa ajili yangu na familia yangu kwa sababu baada ya miaka mitano sina akiba yoyote. Ubunge umenitia umaskini ambao sikuwa nao kabla ya 2010. Hii ni ngumu kuaminika lakini ni kweli kwangu na, ninaamini, kwa wabunge wengi.
Sisi wabunge ni mobile ATMs, whether we like it or we don't.
Pili, kwa sababu chama changu na wagombea wenzangu wa ubunge na udiwani wanazihitaji.
Ni hivi, kwenye uchaguzi uliopita wa vijiji na vitongoji ambako tuliimaliza CCM jimboni kwangu, sehemu kubwa ya gharama nilizibeba mimi na, ninaamini, wabunge wenzangu wa CHADEMA walifanya hivyo majimboni kwao.
Ukweli wa Mungu ni kwamba chanzo kikubwa cha fedha za CHADEMA majimboni ni wabunge wa chama. Wagombea udiwani wetu wanatutegemea sisi wabunge tuwezeshe kampeni zao kwa fedha, magari na vifaa mbali mbali vya uenezi wa chama na kampeni.
Kwa hiyo, choice yetu ni tuchukue ili tupatie vitendea kazi ya ukombozi, au tuache kuchukua tukose pesa za kutuwezesha kushinda uchaguzi ujao. We are not naive, tutazichukua ili tuzifanyie kazi ya kushindia uchaguzi ujao.
Tatu, je tusipozichukua ndio hazitatoka??? Hapana!!! Tusipozichukua bado maCCM watachukua zao na, possibly na zetu pia, na watazitumia kutuchapia kwenye uchaguzi ujao.
Kipi ni afadhali, tuzichukue tushindie uchaguzi au tuziache ziliwe na maCCM halafu tuchapwe kwenye uchaguzi??? Tukumbuke zile za bunge la bajeti tulipotoka hazikurudi hazi zililiwa.
Kwangu mimi ni afadhali kuzichukua, sijui kwako wewe unayesoma message hii. Nne, je tukizichukua tunakuwa mafisadi sawa na maCCM?
Mimi sidhani hivyo kwa sababu nilizozitoa, sijui wewe umasemaje. Wengi wanafikiri wabunge wana hela sana. Wapo wachache sana wenye hela sana, walio wengi ni madeni matupu!
Na hii ni ngumu kuamini lakini mark my words: ni wabunge wachache sana watakaotoka na milioni 100 kati ya hizo tunazosikia tutazilipwa!!! Nyingine zote zitaishia kwenye mabenki!!!! I rest my case.
Tafadhali sambaza kwenye magroup mengine unakoendelea mjadala huu. Nimesahau group niliyowaahidi maelezo haya jana usiku. Wakatabahu.
Tundu Lissu."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni