Lebo

Jumamosi, 30 Mei 2015

Mhe.Edward Lowassa kutangaza nia ya kugombea Urais leo

Katika harakati za Watanzania wengi kujaribu bahati ya kwenda magogoni (ikulu), leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutakuwa na kile kinachoitwa mwanzo wa safari ya matumaini kwa mujibu wa Lowassa mwenyewe na wale wanaojiita marafiki zake.
Maandalizi ya kutekeleza hafla hiyo yamepamba moto na hiyo hapo chini ni picha inayoonesha jukwaa ambalo Mhe.Edward Lowassa atalitumia pindi atakapowahutubia raia watakaofika uwamjani hapo.


Kwa tathmini ya haraka haraka kuhusu gharama za matangazo na maandalizi ya tukio hili, huwezi pata kigugumizi kuelewa kwamba sasa Mhe.Edward Lowassa ameamua kujikita rasmi katika mbio za kuelekea ikulu.
Taarifa za awali zilizosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari, inasemekana kwamba watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamesafiri mpaka Arusha kwa ajiri ya kuhundhuria tukio hili la kipekee. Kwa mantiki ya siasa na propaganda zake, ni dhahiri kwamba danganyatoto ya kisiasa imetumika ili kuwavuta watu kwenda katika viwanja vya Amri Abeid. Nasema hivi kwasababu hakuna takwimu sahihi na zisizo acha shaka kwamba watu kutoka mikoani wameingia Arusha kwa wingi mno kiasi cha nyumba za wageni kujaa na watu kukosa pa kulala. 
Pamoja na mambo mengine, idadi kubwa ya wamasai kutoka Monduli wameonekana mapema katika eneo la tukio wakionesha utayari wa kumuunga mkono mbunge wao kama inavyoonekana katika picha hiyo hapo chini.


Pamoja na mambo mengine, Mhe.Edward Lowassa ni mbunge wa Jimbo la Monduli ambaye pia amewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania tangu mwaka 2005 mpaka 2008. Kwa muktadha huu ni dhahiri alilitumikia taifa kama waziri mkuu kwa kipindi cha miaka mitatu tu, alilazimika kujiuzuru mapema mwaka 2008 kutokana na kutajwa kushiriki katika kashfa ya ufisadi wa kampuni hewa ya kufua umeme almaarufu Richmond.
Mhe.Edward Lowassa alitajwa na kamati maalumu ya bunge chini ya Dr.Harrison Mwakyembe kwamba aliingilia mchakato wa utoaji zabuni kwa makampuni ya kufua umeme jambo lililopelekea kuundwa kwa kampeni hewa la Richmond na hatimaye kuliingizia taifa hasara ya dola za Marekani Milioni 120.
Katika sakata hilo lililotikisa taifa, Mhe.Lowassa alijiuzulu sambamba na mawaziri wengine ambao ni Nazir Karamagi na Mhe.Msabaha ambao pia amewataja kuwa sambamba nao katika kile anachokiita safari ya matumaini.
Pia, mkurugugenzi mstaafu wa idara ya usalama wa taifa ndugu Apson Mwang'onda ametajwa kuwa mmoja wa waratibu wakuu wa harakati za Lowassa kwenda ikulu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni