Lebo

Ijumaa, 3 Julai 2015

Sergio Ramos aipenda Manchester United

Image result for pictures of sergio ramos
SERGIO RAMOS

Wiki moja baada ya ofa ya kwanza ya Manchester United kumsajili Sergio Ramos kukataliwa na Real Madrid, hatimaye mchezaji huyo ambaye yupo mapumzikoni ametoa kauli yake kwamba anaipenda timu ya Manchester United na atafurahi endapo ataanza maisha mapya katika klabu hiyo ya Uingereza.

Mapema wiki iliyopita wakuu wa idara ya usajili wa timu ya Manchester United walitoa ofa ya kumsajili beki huyo wa timu ya Real Madrid kwa kitita paundi milioni 28.3 lakini uongozi wa Real Madrid ulikataa ofa hiyo. Taarifa za ndani kutoka klabuni hapo zinaeleza kuwa Real Madrid bado alikuwa kuwa kwenye mipango ya kuongezewa dau la usajili na Real licha ya kutokumjuza mapema.

 Image result for pictures of sergio ramos

Taarifa za mchezaji Sergio Ramos kujiunga na wakali wa Old Trafford zilisambaa mitandaoni na katika vyombo vingine vya habari baada ya kocha wa timu ya Manchester United, Luis Van Gaal kuweka wazi mipango yake ya kumhitaji beki huyo kwa lengo la kuimarisha safu yake ya ulinzi. 

Pamoja na tetesi kwamba uongozi wa Real Madrid umeweka mkakati wa nguvu wa kumuongezea dau Ramos, kaka wa mchezaji huyo Rene Ramos amenukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa kuna kila haja ya uongozi wa Madrid kuheshimu maamuzi ya mdogo wake ili aende kuanza maisha mapya ndani ya Mashetani Wekundu.

Sergio Ramos mwenyewe ameweka msimamo wake kwamba anataka kwenda united hivyo jambo pekee ambalo uongozi wa Madrid unatakiwa kulifanya ni kukubaliana na Manchester United kuhusu ada ya uhamisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni