Watu 150 wameuawa baada ya Boko Haram kuvamia kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Walioshuhudia mashambulizi hayo wanasema watu tisini na saba wameuawa siku ya Jumatano katika kijiji cha Kukawa kilichopo karibu na Ziwa Chad.Habari zinasema pia wanaume 48 wamepigwa risasi na wapiganaji katika mashambulizi tofauti siku ya Jumanne.
Mashuhuda wanaokimbia eneo lililopo karibu na Ziwa Chad wanasema idadi kubwa ya wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo wameuwa wanaume, wanawake na watoto.Baadhi ya ripoti zinasema walipigwa risasi huku wengine wakielezea jinsi wapiganaji hao walivyowachinja watu na kuchoma majengo.
Upande wa Kusini, nje kidogo na mji wa Monguno, kundi la wapiganaji wa Boko Haram wamefika usiku wakati watu walipokuwa wanaswali. Waliwasubiri mpaka walipomaliza kuswali na kuwatenganisha wanaume na wanawake na baadae kuanza kuwamiminia risasi wanaume.
RAIS WA NIGERIA MUHAMMADU BUHARI |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni