Lebo

Ijumaa, 3 Julai 2015

UHURU KENYATTA ASHINDA TUZO YA RAIS BORA WA AFRIKA MWAKA 2015


 


ushund
RAIS UHURU KENYATTA AKIKABIDHIWA TUZO

 Rais wa Jamhuri ya Watu wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameshinda tuzo ya rais bora wa Afrika kwa mwaka 2015. Tuzo hiyo inayotolewa na jumuiya ya umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika, pamoja na mambo mengine kuna vigezo vya msingi na kimantiki vilivyopelekea Mhe.Uhuru Kenyatta kukabidhiwa tuzo hiyo.

Miongoni mwa vigezo vilivyomfanya kushinda ni pamoja na uwezo wake wa kujenga makubaliano kitaifa na kimataifa na juhudi zake za kubadilisha sera na kutoa ufumbuzi katika masuala yanayohusu nchi ya Kenya. Wadadisi wa mambo ya siasa za Afrika wanaona ya kwamba hali ya utulivu na utayari wa kukabiliana na changamoto katika taifa pasipo kutegemea msaada mkubwa wa hali na mali ndicho kichocheo kikubwa katika ushindi huo.

Pia jitihada zake katika kuboresha elimu ya umma na kusimamia utekelezaji wa katika mpya ya Kenya ni moja ya mafanikio makubwa yanayomtofautisha Rais Kenyatta na viongozi wengine barani Afrika. Kabla ya hapo tuzo ya Rais Bora Wa Afrika alikabidhiwa Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia alitajwa kufanikiwa sana katika kuliunganisha taifa lililokuwa limemeguka kwa misingi ya ukabila kati ya Wahutu na Watutsi.

 Image result for PICTURE OF UHURU KENYATTA

Ikumbukwe kwamba kabla ya kusimama vema kama rais wa jamhuri na kutekeleza majukumu yake kwa uhuru mkubwa, rais Kenyatta alikabiliana na changamoto kubwa ikiwamo ya kukabiliana na kesi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu huko The Hague, Uswisi katika mahakama ya International Criminal Court (ICC) kabla ya kufutwa rasmi mapema mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa sasa changamoto kubwa anayokumbana nayo Rais Uhuru Kenyatta ni kuimarisha usalama wa Kenya haswa kutokana na matukio ya kigaidi yanayotekelezwa na kikundi cha kigaidi kutoka nchini Somalia almaarufu Alshaabab. Miezi michache iliyopita, idara ya usalama wa kijeshi nchini Kenya na Tanzania zilikutana hii ilikuwa ni baada ya Kenya kuomba msaada wa mbinu za kukabiliana na magaidi kutoka JWTZ. Matumaini ya usalama kuimarika nchini Kenya ni makubwa kwa siku zijazo, ni suala la kuomba Mungu na kutekeleza wajibu wa kiusalama na kiraia kwa wakaaji wote wa Afrika ya Mashariki.

PONGEZI RAIS UHURU KENYATTA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni