Lebo

Ijumaa, 3 Julai 2015

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI IMETAJA MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI, SOMA HAPA


 Image result for NEMBO YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

1.Buhigwe-Kigoma
2.Uvinza-Kigoma
3.Kakonko-Kigoma
4.Butiama-Mara
5.Chemba-Dodoma
6.Ikungi-Singida
7.Itumila-Simiyu
8.Kaliua-Tabora
9.Mbogwe-Geita
10.Mkalama-Singida
11.Mlele-Katavi
12.Momba-Mbeya
13.Ngang'hwale-Geita
14.Nyasa-Ruvuma
15.Wanging'ombe-Njombe.

Majimbo mengine yatatajwa siku kadhaa zijazo.


Pamoja na hayo ifahamike vema kwamba miongoni mwa majukumu ya tume ya taifa ya uchaguzi ni haya yafuatayo:

(a) Kusimamia na Kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(b) Kusimamia na Kuendesha Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(c) Kupitia na Kugawa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi wa Wabunge.

(d) Kusimamia na Kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura na kuendesha Uchaguzi wa Madiwani Tanzania Bara.

(e) Kutangaza matokeo ya Viti Maalum vya wanawake vya Ubunge na Udiwani.

(f) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura na kusimamia Watu na Asasi zitakazohusika katika Kutoa Elimu hiyo.

(g) Kutekeleza Majukumu mengine yatokanayo na Sheria itakayotungwa na Bunge.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni